tangazo

Mandamano ya ghadhabu yasambaa Marekani kufuatia mauaji ya mtu mweusi

Maandamano nchini Marekani kuhusu mauaji ya mtu mweuzi George Floyd aliyefariki baada ya kukoseshwa pumzi na maafisa wa polisi katikati ya barabara wiki hii mjini Minnessota, yameenea katika taifa hilo siku ya Ahamisi jioni huku visa vya ghasia vikisambaa.

Maandamano yaliosababisha ghasia za Mineapolisi zilizosababisha srikali ya jimbo hilo kupelekea kikosi cha kitaifa cha ulinzi yalienea hadi katika majimbo mengine huku mamia ya watu wakiandamana katika jimbo la California, Chicago, Memphis , New York , Okaland , Ohio na Colorado.
Kumekuwa na ghadhabu za 'i cant breath'{Siwezi kupumua} nchini Marekani kuhusu kifo cha Mmarekani huyo mweusi baada ya kukamatwa na polisi.
Na kufuatia maandamano hayo, Denver Capitol ilifungwa kwa dharura baada ya mtu mmoja kuwafyatulia risasi waandamanjiijapiokuwa kulingana na maafisa wa polisi hakuna majeraha yalioripotiwa.
Mamlaka ya LouisVille, Kentucky ilithibitisha kwamba takriban watu saba walijeruhiwa mmoja wao akiwa katika hali mahututi , wakati wa ufyatuaji mwengine wa risasi.
ProtestasHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMaandamano haya yameendelea kwa usiku wa tatu mfululizo huku baadhi ya waandamanaji wakichoma moto kituo cha polisi
Baadhi ya majengo yalichomwa moto na kuibiwa na baadhi ya waandamanaji
Wakati huohuo , takriban watu 40 walikamatwa wakati wa maandamano yaliosambaa katika eneo lote la kusini mwa Manhatta, kulingana na mamlaka
Waandamanaji wakichoma kituo cha polisi cha Minneapolis
Vyombo vya habari vinasema kwamba maandamano tofauti yalifanyika katika maeneo tofauti ya mji siku nzima huku mjini Los Angels watu kadhaa wakishambulia gari la maafisa wa polisi.
Hatahivyo kiwango kikubwa cha maandamano hayo kwa siku ya tatu mfululizo yalifanyika katika eneo la St Paul lililopo mji mkuu wa Minnesota na miji mingi ya jimbo hilo.
Kulingana na ripoti za vyombo vya habari , waandamanaji walivunja kituo cha polisi cha Minneapolis na kukichoma, hatua iliofanya maafisa wa polisi katika kituo hicho kuondoka kwa haraka.
MinneapolisHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBaadhi ya majengo yakichomeka
Nini kinachoendelea Minnesota?
Siku ya Jumatano, kwa mfano , baadhi ya mamia ya waandamanaji walirusha mawe na kukivamia kituo hicho cha polisi ambapo maafisa wa polisi walikizunguka ili kukilinda dhidi ya waandamanaji.
Pia kulikuwa na wizi wa maduka na vitendo vya uvunjani pamoja na makabiliano na maafisa wa polisi waliotumia vitoa machozi na risasi bandia kuwatawanya waandamanaji.
Visa hivyo vilirejelewa siku wa kuamkia siku ya Ijumaa.George Floyd, Mmarekani mweusi mwenye umri wa miaka 46 alifariki siku chache zilizopita baada ya ya kukamatwa na polisi.
George FloydHaki miliki ya pichaTWITTER/RUTH RICHARDSON
Image captionGeorge Floyd alisema mara kadhaa kwamba anashindwa kupumua.
kanda ya video iliochapishwa baadaye ilionyesha kwamba hakuweza kupumua akiwa sakafuni huku afisa mmoja wa polisi akimwekea goti lake katika shingo yake.
Maafisa wanne wa polisi tayari wamefutwa kazi
Meya wa mji huo Jacob Frey alisema kwamba 'kuwa mtu mweusi sio hukumu ya kifo' na kutoa wito kwa maafisa hao wa polisi kufunguliwa mashtaka katika kanda hiyo ya video.
Gavana wa Minnesota Tim Walz aliwapeleka maafisa wa kikosi cha kitaifa cha ulinzi kukabiliana na waandamanaji siku ya Alhamisi , akitangaza hali hiyo kuwa ya dharura.
Alisema kwamba wizi, uvunjaji na uchomaji moto ulisababisha uharibifu kwa kampuni nyingi.

Post a Comment

0 Comments