tangazo

Marekani yarekodi idadi ya chini ya vifo vya COVID-19 kwa siku ya pili

Marekani imeingia siku ya pili mfululizo ikiwa na idadi ya chini ya vifo zaidi ya 900 vya COVID-19, wakati shirika la afya duniani WHO likisifu maendeleo yaliyopatikana duniani, lakini limeonya juu ya hitaji la umakini mkubwa dhidi ya wimbi la pili la maambukizi ya virusi hivyo.

Hadi sasa virusi vya corona vimewaua watu zaidi ya 285,000 huku idadi ya maambukizi ikipindukia watu milioni 4.1 duniani kote.

Mkurugenzi wa shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema kiwango cha maambukizi katika nchi nyingi kimeanza kupungua, kutokana na hatua za kufunga nchi zilizoanzishwa na mataifa mengi.

Barani Ulaya ambako viwango vya maambukizi na vifo vilikuwa vikubwa, mamilioni ya watu wameanza kurejea katika shughuli za kawaida.


ADVERTISEMENT

Post a Comment

0 Comments