tangazo

Mbaya wa Simba, Yanga na Azam kujulikana leo

LEO Mei 29 mbivu na mbichi zitajulikana kwa kila timu iliyotinga atua ya robo fainali kutambua itakutana na nani kwenye mchezo wao unaofuata.

Bingwa mtetezi wa Kombe la Shirikisho ni Azam FC ambaye alitwaa kombe hilo kwa kumtungua bao 1-0 Lipuli bao lililopachikwa kimiani na Obrey Chirwa.

Majira ya saa tano asubuhi droo itachezwa ili kila timu itambue nani atacheza naye.

Timu nane zilitinga hatua ya robo fainali ambazo ni Yanga Alliance FC, Azam FC, Kagera Sugar, Namungo FC, Ndanda FC na Simba hizi zipo Ligi Kuu Bara huku Sahare All Stars inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Post a Comment

0 Comments