tangazo

Mbunge CHADEMA 'akanusha' kukiuka agizo la Mbowe

Mbunge wa Viti maalum, CHADEMA, Cecilia Paresso amekanusha taarifa za yeye kuhudhuria Bungeni siku ya jana na ameshangazwa kuona jina lake limetajwa kwenye idadi ya wabunge 11 waliohudhuria Bungeni kinyume na tamko la Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe.

 Paresso amesema si kweli kama na yeye alishiriki kikao cha Bunge jana, kama ambavyo imeripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini.

Mbali na Paresso Wabunge wengine ambao walionekana kushiriki kikao cha jana cha Bunge, ni Mbunge wa Kilombero Peter Lijualikali, Mbunge wa Mbozi David Silinde, ambao wao picha zao zilionekana.

Wabunge wengine ambao wanadaiwa kushiriki kikao hicho, licha ya picha zao kutoonekana ni Wabunge wa Viti maalum ambao ni Suzan Masele, Joyce Sokombi, Latifa Chande, Mbunge Jafari Michael jimbo la Moshi Mjini, Anthony Komu jimbo la Moshi Vijijini.

Kwa upande wao CHADEMA wameeleza kuwa wanafuatilia kwa ukaribu ili kupata maelezo kamili, kwanini Wabunge hao walifanya maamuzi kinyume na chama chao na watatangaza hatua watakazochukuliwa.

Post a Comment

0 Comments