Mbunge Koka akabidhi baiskeli 95,barakoa, ndoo na sanitizer kwa viongozi wa matawi CCM

MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Mjini, Silvestry Koka, amekabidhi baiskeli 95 zenye thamani ya sh.milioni 25 kwa viongozi wa matawi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jimboni humo ,kwa ajili ya urahisishaji wa utendaji kazi.


Aidha Koka ametoa ndoo za Maji,dawa ya kunawia mikono “Sanitizer” na barakoa zenye thamani ya sh.milioni 3 kwa ajili ya kutumika katika Ofisi za Chama za matawi na kata na kuwakumbusha kujihadhari dhidi ya Ugonjwa wa Virusi vya Corona (Covid 19).


Akizungumza wakati wa makabidhiano ya baiskeli hizo ,Kata ya Pangani, Maili Moja na Tumbi , alisema ameamua kutoa vitendea kazi hivyo Ili kurahisisha utendaji kazi kwa viongozi wa Chama hicho kuwafikia wanachama.

“Wakati wa mkutano mkuu wa CCM wa wilaya niligawa pikipiki 14 kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa makatibu wa kata lakini  nimekabidhi baiskeli 95 kila moja Sh. 250,000 kwa ajli ya viongozi wa matawi;.

Mbunge huyo ,aliisihi jamii kufuata elimu inayotolewa na wataalamu wa afya ,kunawa mikono ,kujikinga na barakoa ,kuwalinda watoto ,kuacha mikusanyiko pamoja na kuacha kupeana mikono ,na wajifukize ili kupambana na ugonjwa wa corona.

Nae mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kibaha Mjini, Maulid Bundala alieleza ,pikipiki na baiskeli ni vitendea kazi na mali ya Kata na Tawi la Chama Cha Mapinduzi (CCM) isifike mahali wakatumia vitendea kazi hivyo kuwanufaisha katika shughuli zao binafsi .

Katibu wa CCM Kibaha Mjini, Afidu Luambano alisema wajipanga kushinda uchaguzi mkuu kwa kishindo hivyo aliwahimiza wanachama wa CCM wakajiandikishe na kusahihisha majina katika daftari la kupiga kura,kwa kuhakiki majina kama  yapo ili wapate ridhaa ya kupiga kura lakini pia wakumbuke kulipia ada ya kadi zao.

Post a Comment

0 Comments