tangazo

Mbunge wa CCM akamatwa na bunduki 10, risasi 536

Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia Mbunge wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Suleiman Masoud Suleiman “Nchambi” (CCM) kwa tuhuma za kumiliki silaha 10, risasi 536 na nyama zinazodhaniwa kuwa ni za wanyawapori kinyume cha sheria.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Kamishna msaidizi wa Polisi Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea Mei 3,2020 majira ya saa sita kasoro usiku katika mtaa wa Lubaga Manispaa ya Shinyanga.

Post a Comment

0 Comments