Mfahamu mwanamziki Davido kiundani zaidi


Novemba 21, 1992 alizaliwa mwanamuziki wa Nigeria, prodyuza na mtunzi wa nyimbo maarufu Davido.

Jina lake halisi ni David Adedeji Adeleke. Alizaliwa Atlanta katika jimbo la Georgia nchini Marekani na kukulia jijini Lagos nchini Nigeria.  Davido aliutambulisha muziki wake akiwa na kundi la muziki la KB International.

Davido katika masuala ya elimu hayuko mbali, alikwenda kuchukua Shahada yake ya Utawala katika Biashara kwenye Chuo Kikuu cha Oakwood kabla ya kuiweka pembeni na kujikita katika masuala ya muziki.

Davido aliibuka mnamo mwaka 2011 alipoachia kibao cha Dami Duro, baadaye alirudi na albamu mwaka mmoja baadaye ya Omo Baba Olowo. Katika albamu hiyo nyimbo sita ndani yake zilimpa kufahamika zaidi : "Back When", "Ekuro", "Overseas", "All of You", "Gbon Gbon", na "Feel Alright". Kati ya mwaka 2013 na 2015 aliachia singo singles "Gobe", "One of a Kind", "Skelewu", "Aye", "Tchelete (Goodlife)" akimshirikisha Mafikizolo, "Naughty" akimshirikisha DJ Arafat, "Owo Ni Koko", "The Sound" na "The Money" akimshirikisha Olamide. Mano Januari 2016 Davido alitangaza katika mtandao wa Twitter kuwa amesaini mkataba na Sony Music.

Tangazo hilo lilitoa hisia tofauti katika ulimwengu wa muziki. Miezi michache baada ya kutolewa kwa tangazo hilo Davido alionekana akifanya kazi na lebo ya DMW ambayo ni Davido Music Worldwide. Wasanii kama Dremo na Mayorkun wanafanya kazi chini ya lebo hiyo.

Mnamo Julai 2016 Davido alisaini mkataba chini ya lebo ya Sony’s RCA Records. Akiwa na lebo hiyo ametoa nyimbo tano pia amefanya kazi na wasanii wengine kama Simi, Tinashe na Nasty C.

Mwaka 2017 nao ulikuwa mwaka mzuri kwake akiachia ngoma nyingine tano zikiwamo za “If” na “Fall”. Davido ameweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza wa Nigeria katika category ya Pop kukaa katika Billboard muda mrefu.

Post a Comment

0 Comments