tangazo

Mike Tyson kurudi tena ulingoni

Bingwa wa zamani wa ndondi katika uzito wa juu duniani, Iron Mike Tyson,  yupo katika mazoezi makali ya kurudi jukwaani, akitaka kucheza pambano la raundi tatu hadi nne.

Chini ya mkufunzi wake, Rafael Cordeiro, Tyson baada ya kuposti video hiyo fupi katika ukurasa wake wa #Instagram ameonekana kuwa mwepesi katika mazoezi yake yaliyowashangaza watu zaidi ya milioni moja kutokana na kasi yake.

Mike Tyson (53) anatarajiwa kurudi ulingoni katika pambano maalum la kuchangisha fedha na litakuwa la raundi zisizozidi tano, lakini mpinzani wake bado hajaulikana.

Post a Comment

0 Comments