tangazo

Misikiti, shule kufunguliwa Korea Kusini

Waislamu nchini Korea Kusini wameamua kufungua tena misikiti ifikapo Jumatano, kwani hakuna kesi mpya ya maambukizi ya virusi vya corona iliyoripotiwa nchini humo ndani ya siku tatu mfululizo.

Wakionyesha ujasiri mkubwa katika kuushinda ugonjwa mbaya zaidi wa COVID-19, Waislamu nchini Korea Kusini Jumatatu walitangaza kufungua misikiti kwa ajili ya ibada.

Kulingana na taarifa ya Shirikisho la Waislamu la Korea Kusini la Seoul,misikiti itafunguliwa kwa ajili ya sala ya taraweh maalumu katika mwezi mtukufu wa Ramadhan na vilevile sala ya Ijumaa.


Shirikisho hilo, hata hivyo, limewataka Waislamu wa nchi hiyo kufuata hatua za serikali dhidi ya COVID-19 na kudumisha umbali wa mita moja wakati wa sala.

"Waislamu wote wanapaswa kufuata masharti yote ambayo yanaweza kuzuia kuenea kwa COVID-19," iliongezea taarifa hiyo.

Kufuatia mlipuko wa corona,serikali iliwataka waumini wa dini kuepuka mikusanyiko ili kusaidia kupunguza kusambaa kwa virusi hivyo.

Waislamu wametakiwa kutumia sanitizer,kuvaa barakoa na kujisajili kabla ya kuingia misikitini.

Serikali pia imeamua kuanza kufungua shule hatua kwa hatua kuanzia wiki ijayo.

Vituo vya Korea vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa vilisema idadi ya jumla ya kesi zilizothibitishwa imeongezeka hadi 10,801 baada ya kuongezeka kwa kesi nane za maambukizi siku ya Jumatatu.

Wagonjwa wengine wawili wamepoteza maisha kutokana na virusi hivyo,hali iliyopelekea idadi ya vifo kufikia 252.

Wagonjwa wengine  9,217 wamepona na kuwafanya jumla ya 85% ya watu walioambukizwa kupona nchini humo.

Korea Kusini imefanya vipimo 633,921 tangu Januari 3.

Post a Comment

0 Comments