tangazo

Mnyama anayesambaza virusi vya corona

Kuna mnyama aliyesambaza virusi vya corona kutoka kwa popo hadi kwa binadamu, utafiti unaonesha.

Lakini wakati ambapo Shirika la Afya Duniani linasema utafiti huo umelenga chimbuko la virusi hivyo, baadhi ya wanasayansi wanasema huenda isifahamike vile mtu wa kwanza alivyoambukizwa.

Bado haijafahamika ikiwa mnyama aliyesambaza virusi hivyo aliuzwa katika soko la wanyama pori la Wuhan nchini China ambalo kwa sasa limejitia dosari.

Lakini biashara ya wanyama pori inaonekana kama chanzo cha virusi hivi.

Watafiti wanasema biashara ya wanyama pori inatoa fursa ya usambaaji wa magonjwa kutoka kwa spishi moja hadi nyengine ambako kulisababisha milipuko kadhaa iliyopita na imelaumiwa kwa janga hili la corona.

Afisa wa Shirika la Afya Duniani anayehusika na utafiti wa Covid-19, Dkt. Maria Van Kerkhove, ameiambia BBC katika kipindi cha Andrew Marr show: "Tunajitayarisha kukabiliana na janga kama hili kwasababu sio suala la ikiwa linaweza kutokea, badala yake ni lini litatokea."

Wataalamu wa magonjwa ya kuambukiza wanakubali kwamba kama magonjwa mengine yanayojitokeza, virusi hivi awali vilisambaa bila kugundulika kati spishi moja hadi nyengine.


Profesa Andrew Cunningham, kutoka Chama cha Hifadhi ya Wanyama cha Uingereza, anaelezea: "Kwa muda mrefu tumekuwa tukitarajia kuwa kitu kama hiki kinaweza kutokea.

"Magonjwa kama haya yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara katika miaka ya hivi majuzi kwasababu ya wanadamu kuvamia makao ya wanyama hao na kuongezeka kwa utangamano na watu kutumia wanyama pori."

Virusi vinavyosababisa Covid-19 havijakaribiana na mlipuko wa kwanza wa virusi kama hivyo. Inaingia kwenye orodha ya vinavyosababisha magonjwa kama vile Ebola, kichaa cha mbwa, Sars na Mers - ambayo chanzo chake ni popo wa mwituni. Baadhi ya ambayo kwasasa hivi ni ushahidi kuhusu virusi vya popo na uwezo wa kuambukiza mwanadamu kunatokana na utafiti wa mlipuko wa ugonjwa wa Sars uliotokea 2003 wenye uhusiano wa karibu na virusi vya corona.
Kinachohitajika kwa virusi ili viweze kuambukiza mtu mwengine mpya ni uwezo wa chembe kuingia ndani na kuanza kuzaliana.

Na kama ilivyo kwa ugonjwa wa Sars, popo mwenye kusemekana kuwa chanzo cha virusi vya corona alikuwa na uwezo wa kuingia kwenye seli za binadamu.

"Kwa ugonjwa wa Sars-CoV-2 cha msingi ni protini ya virusi inayoitwa Spike na ili kuweza kuingia kwenye seli au chembe unahitaji kipokezi mfano wa funguo katika usemi wa kawaida. Kipokezi hicho kinajulikana kama ACE2," ameelezea Profeesa David Robertson, mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza kutoka chuo kikuu cha Glasgow.

"Virusi vya corona sio kwamba vinaweza kuingiliana vizuri na kipokezi cha ACE2, "Hali hii imekuwa ikitokea mara nyingi hata kuliko virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Sars-1", amesema.

Na kwasababu hiyo, ni wazi kwamba virusi vya corona ni rahisi sana kusambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwengine; ni ugonjwa wa kuambukiza ambao umekuwa changamoto kudhibitika. Lakini hadi kuleta karibu virusi vya popo kwa seli ya mwanadamu hapo ndipo biashara ya wanyama pori inaposemekana ilichangia kwa kiasi kikubwa sana.

Post a Comment

0 Comments