Mshauri mkuu wa Rais wa Congo afunguliwa mashtaka ya rushwa

Mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa ambaye pia ni mshauri mkuu wa Rais Felix Tshisekedi amefunguliwa mashtaka nchini Congo jana.

Vital Kamerhe ambaye amekuwa katika kitovu cha siasa za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kwa miongo miwili, anatuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha kiasi cha dola milioni hamsini.

 Kamerhe mwenye umri wa miaka 61 aliwasili katika eneo la gereza kuu la Kinshasa akiwa amevalia mavazi ya jela ambako amekuwa akizuiliwa tangu mnamo Aprili 8.

Washtakiwa wengine wawili katika kesi hiyo, mfanyabiashara mmoja kutoka Lebanon na afisa mmoja katika afisi ya rais pia walifikishwa eneo hilo katika kusikilizwa kwa mara ya kwanza kwa kesi hiyo iliyopeperushwa moja kwa moja na televisheni ya taifa nchini humo RTNC.

Wafuasi wa Kamerhe wanasema kesi hiyo imechochewa kisiasa na inanuia kumzuia asigombee urais katika uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika katika kipindi cha miaka mitatu.


ADVERTISEMENT

Post a Comment

0 Comments