tangazo

Mtoto wa Miezi 6 Akutwa na Virusi vya Corona

WIZARA ya Afya nchini Kenya imetangaza ongezeko la visa 25 vya #COVID19 baada ya sampuli 1,012 kufanyiwa vipimo na kufanya idadi ya visa nchini humo imefikia 490 huku wagonjwa 6 zaidi wamepona na jumla ya waliopona ni 163.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya nchini humo, Mercy Mwangangi, amesema wagonjwa wapya ni raia wa Kenya wenye umri kati ya miezi 6 na miaka 60 na watu 13 ni wanaume na 12 ni wanawake, wote hawana historia ya kusafiri hivi karibuni.

Katibu huyo ameeleza kuwa wanafanya kazi na wataalamu mbalimbali wa afya na kuhusu watoto wenye corona virus, amesema wizara itashirikiana na wataalamu wa magonjwa ya atoto.

Kuhusu posho za watumishi wa afya, Mwangangi amesema hakuna upendeleo na watahakikisha kila mmoja anapata stahiki yake. Tamko hilo linakuja baada ya umoja wa kitaifa wa wauguzi kutoa notisi ya mgomo wa siku 14 kwa madai kuwa hakuna usawa kwenye ugawaji wa posho.

Post a Comment

0 Comments