Mwananchi apanga kufungua shauri, Mahakama izuie uchaguzi mwaka huu

Na Amiri kilagalila,Njombe
Mwananchi mmoja anaefahamika kwa jina la Johnson Mgimba mkazi wa Njombe Mjini amesema kutokana na ugonjwa wa covid19 kuendelea kushika kasi nchini na duniani kote , amekusudia kufungua kesi katika mahakama kuu kanda ya Iringa ya kuomba serikali kusitisha mchakato na maandalizi ya uchaguzi mkuuu na fedha iliyotengwa kuelekezwa katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Raia huyo ambaye amejibatiza jina la kijana mzalendo amesema kuna kila sababu ya kusitisha uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu ili kutoa nafasi kwa viongozi waliopo madarakani sasa kuendeleza jitihada ambazo wameanza kuzichukua katika kukabiliana na ugonjwa huo ambao hadi sasa nchini kuna visa visivyopungua 480.


Mgimba anasema fedha iliyokuwa imetengwa na serikali kwa ajili ya kutekeleza shughuli za uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani ni vyema ikaelekezwa katika kununua vifaa vya kupimia corona,mashine za kupumulia wagonjwa,dawa na vifaa vya kinga ili kunusuru maisha ya wagonjwa wengi ambao wamekuwa katika hatari ya kupoteza maisha kutokana na huduma duni.

“Nikiwa kama mtanzani sioni sababu ya kuendelea na harakati za uchaguzi,ninaenda kufungua shauri Mahakamani la kuiomba Mahakama la kuiomba mahakama kuzuia shughuli za uchaguzi kwa kuwa kwa gonjwa hili (Corona) linavyoenda ninaona kuna kila sababu ya kusitishwa uchaguzi hadi hali itengamae”Johson Mgimba Mkazi wa Njombe mjini

 “Gonjwa hili la Corona linaendelea kututafuna,ninataka niiombe Mahakama yetu ya Tanzania iweze kuzuia uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na badala yake fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya uchaguzi ziingie kwenye vita ya kupambana na Corona,ni swala tu Mahakama ione namna ya kuwaongezea muda viongozi waliopo” Johson Mgimba Mkazi wa Njombe mjini

Katika hatua nyingine mwananchi huyo ametoa pendekezo lake kwa serikali la kutangaza majina ya wahanga wa ugonjwa huo tishio ulimwenguni  ili kuwafanya wananchi wengine kuchukua hatua za haraka za kwenda kupima endapo mtu wao wa jirani atabainika kuwa na ugonjwa huo

“Kwasababu ugonjwa wa Corona sio wa aibu,ni kweli sheria hairuhusu mgonjwa kutangazwa,lakini kwa ugonjwa huu badala ya kutumia nguvu kubwa kutafuta watu waliokutana na yule mgonjwa wa Corona basi wagonjwa wale watangazwe kwa majina kwasababu wale waliokutana na mgonjwa kwa haraka watasimama wenyewe kuelekea vituo vya afya” Johson Mgimba Mkazi wa Njombe mjini


Hivyo mei 5 kijana huyo aliyejipa jina la mzalendo amewataka wananchi wengine wenye mtazamo kama wake kuungana nae siku ya jumanne katika mahakama kuu ya mkoa wa Iringa

“Nitumie wito huu kuwaomba watanzania wote wanaoniunga mkono katika hoja ya kufungua shauri mahakamani juu ya kusitisha shughuli za uchaguzi mkuu mwaka huu,Shauri hili nitakwenda kufungua katika mahakama kuu ya kanda pale Iringa 5/5/2020” Johson Mgimba Mkazi wa Njombe mjini.


Mwezi Machi 26 Mwaka Huu Rais wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli Alisema Uchaguzi Mkuu Hautaahirishwa Kwa Sababu ya Ugonjwa wa Corona.

Hata hivyo ripoti ya mwisho ya april 29 mwaka huu juu ya visa vya corona nchini Tanzania vinapindukia 480,vifo 16 na waliopona ni 167 huku taifa la Marekani likiongoza kwa  kuwa na wagonjwa wengi zaidi duniani wanaofikia zaidi ya milioni moja na vifo 65782 kwa taarifa za saa 24 zilizopita.

Post a Comment

0 Comments