Nyota Jerry Stiller wa Marekani aaga dunia

Nyota Jerry Stiller (kushoto) na mkewe Anne Meara. REUTERS/Phil McCarten/File Photo - RC2AMG94VMMR

Nyota mchekeshaji kwenye jukwaa, filamu na televisheni Jerry Stiller amefariki akiwa na umri wa miaka 92.

Mwanawe, muigizaji Ben Stiller, amesema baba yake alifariki mapema Jumatatu kutokana na sababu za kawaida.

Ben Stiller
Ben Stiller

Stiller alijipatia umaarufu miaka ya 1960 alipoungana na mkewe Anne Meara katika uchezaji filamu, kuigiza kwenye majukwaa, kushiriki katika matangazo ya biashara na programu za televisheni, likiwemo onyesho la Ed Sullivan.

Alipata umashuhuri tena miaka ya 1990 alipoigiza michezo ijulikanayo kama Cranky, Frank Costanza katika show ya Seinfeld iliyokuwa ikionyeshwa katika televisheni.

Fani yake Stiller ilihusisha nafasi alizoigiza katika maonyesho mbalimbali ya Broadway kama vile The Ritz na Hurlyburly, na pia filamu zilizopata umashuhuri Hairspray na Zoolander.

ADVERTISEMENT

Post a Comment

0 Comments