Serikali yatangaza masharti ya mashabiki viwanjani


Serikali imetoa mwongozo wa namna ya wadau wote watakavyoshiriki michezo na ni muhimu kwa wote kuufuata maana unawahusu kuanzia wachezaji, makocha, viongozi na mashabiki.

Hayo yameelezwa na Msemaji mkuu wa serikali Dkt. Hassan Abbas leo Mei 31, 2020 wakati anaongea na waandishi wa habari ambapo amesema Serikali imeridhia ligi zote za soka zichewe kwa mtindo wa kawaida kama ilivyokuwa kabla ya Covid-19 hivyo mechi za Ligi kuu na madaraja mengine zitachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.

''Serikali imeridhia mashabiki watakaotaka kwenda uwanjani wahudhurie mechi kama ilivyokuwa awali lakini wazingatie kukaa mita moja wakati wa kuingia na kuangalia mechi uwanjani, kuvaa barakoa pomoja na viwanja kuwekewa maji tiririka ili wanawe'', amesema Dkt. Hassan Abbas.

Aidha amesema kwa mechi kubwa ambazo zinaweza zikasababisha uwanja kujaa na ile kanuni ya mashabiki kukaa mita moja isizingatiwe, serikali imeagiza utaratibu wa kuingia mashabiki nusu ya uwezo wa uwanja husika ili kuendelea kuchukua tahadhari.

Kwa upande wake Rais wa TFF Wallace Karia amesema, 'Sisi kama TFF tunaishukuru Serikali kwa kuruhusu michezo kurejea na tutazingatia kanuni za usalama wa afya ambazo zimetolewa na niwaombe wadau wakiwemo mashabiki wazingatie sana''.

Bofya hapa kusoma Habari zote

Post a Comment

0 Comments