Shilole ajipanga kupunguza vifo vya akina mama

Staa wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘shilole’ amesema kuwa amejipanga kutengeneza baba bora 2020 na kupunguza vifo vya wakina mama kupitia jukwaa la ‘Tunaweza’.

Akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es salaam baada ya kutangazwa rasmi kuwa balozi wa jukwaa la Tunaweza kupitia taasisi ya smart generation inayolenga kutoa elimu pamoja na kubadili mitazamo mibaya kwa vijana na jamii kwa ujumla.

Amesema akiwa kama mama yupo tayari kupunguza idadi kubwa ya vifo vitokanavyo na uzazi hasa kwa wakina mama wakati wa kujifungua.


“Nina watoto wawili, najua changamoto kwa wakina mama wakati wa kujifungua hivyo vifo vinaweza kuepukika endapo mama atafata taratibu kutoka kwa mtoa huduma yani muuguzi ,”amesema shilole.

Aidha mefafanua zaidi namna dhana iliyojengeka katika jamii juu ya baba kijacho kumsindikiza mama kijacho hospitali ni ushamba au kujishusha thamani hivyo kwa kutumia kampeni hiyo atahakikisha wanaume wote wanaweza na wanahakikisha wanafika hospitali wakiwa na wenza wao .

“Kumpeleka mke au mtarajiwa wako kituo cha afya si ushamba bali ni kuonyesha thamani na hali ya kujali mwenza wako pamoja na mtoto mnaetarajia kumpata huku kufata maelekezo yanayotolewa kituoni hapo na kuchukua tahadhari Kama kumkinga dhidi ya magonjwa hasa maralia,”

Pia ameeleza namna jinsi watu wote watakavokua wanapata elimu jinsi ya kuwa baba bora,mama Bora na kuwakinga wamama wajawazito na magonjwa hasa maralia,kifaa cha mimba,virusi vya ukimwi na mengine.

“Kutokana na ugonjwa wa virusi vya corona (covid 19) ulivoingia na unavoendelea kuwachukua wapendwa wetu hatuna budi kutoa elimu kupitia radio , mitandao ya kijamii pamoja na filamu fupi fupi kupitia Tv ili kuepuka misongamano,”amesema shilole.

Post a Comment

0 Comments