Shirika la UNICEF latoa wito wa msaada wa dola bilioni 1.6 kwa ajili ya watoto

Shirika linaloshughulikia masuala ya watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limetoa wito wa mchango wa dola bilioni 1.6 hiyo ikiwa ni zaidi ya mara mbili ya kiasi cha pesa ilichoitisha miezi miwili iliyopita ili kuwasaidia watoto wanaokumbwa na mizozo ya kibinadamu na ambao kwa sasa wanapambana na virusi vya corona.

UNICEF imesema kuanzia mwezi Machi, imepokea dola milioni 215. Watu milioni nne kote duniani wameathirika na virusi vya corona huku zaidi ya watu 282,000 wakifariki dunia kutokana na ugonjwa huo wa mapafau.Shirika hilo la Umoja wa Mataifa linafanya kazi katika nchi ambazo zinakabiliwa na mizozo ya kibinadamu kwa kuzuia kuenea kwa virusi vya corona na kupunguza athari ya virusi hivyo kwa uwezo wa raia kupata matibabu, chakula, maji, elimu na ulinzi.

 Utafiti wa UNICEF umeonyesha kwamba watoto bilioni 1.8 wanaishi katika mojawapo ya nchi 132 ambazo zina baadhi ya vikwazo vilivyowekwa na serikali kwa ajili ya kupambana na virusi vya corona


ADVERTISEMENT

Post a Comment

0 Comments