tangazo

Sikulazimishwa kuzaa nawe usizae kama haujajipanga- Hamisa Mobetto

Licha ya kwamba Star wa kike Hamisa Mobetto  amezaa Watoto wawili nje ya ndoa, bado ana imani kupitia Ubalozi alioupata kwenye ‘kampeni ya sitetereki’ ataweza kuwasaidia wengine wenye mitazamo tofauti kuhusu afya ya uzazi.

“Sikulazimishwa kuzaa nilikuwa nipo tayari na nilijipanga ndio maana nipo hapa kuwaambia kuwa sio rahisi, usizae kama hauko tayari au haujajipanga, tamaduni zetu tumezoea matunzo anatoa Baba"-Hamisa

Mobetto ametoa kauli hiyo leo wakati akipewa Ubalozi wa ‘kampeni ya sitetereki’ inayosimamiwa na kampuni ya Smart Generation inayoongozwa na Nikk wa Pili  na Mtangazaji Cza wa Clouds FM.

Hamisa anakua Balozi wa Pili baada ya Msanii Nandy  kutambulishwa kama Balozi hivi karibuni.

Post a Comment

0 Comments