tangazo

Singida yafanya maombi kushukuru ahueni ya corona


Vijana wa Mkoa wa Singida, Mwalimu Frederick Ndahani ameongoza waumini wa Kanisa

Katoliki ambao ni marafiki wakubwa wa Mtakatifu ‘Rita wa Kashia’ mkoani hapa
kwenye maombi maalumu ya shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa namna anavyoendelea


kuwalinda na kuwaepusha watanzania dhidi ya madhara yatokanayo na janga la

Covid- 19


Ndahani,
ambaye alimwakilisha Mkuu wa , Dkt. Rehema Nchimbi kwenye kusanyiko la maombi hayo
yaliyofanyika jana eneo la Sukamahela, wilaya ya Manyoni mkoani hapa,
linalosadikiwa kuwa kati kati ya Tanzania, eneo ambalo Kanisa Katoliki limejenga
kituo cha hija kwa heshima ya Bikira Maria“Tumekuja hapa
kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa namna anavyoendelea kulipigania taifa letu kupitia
maombezi ya Bikira Maria dhidi ya janga la corona. Na tumeamua kufanya maombi yetu
eneo hili kwa sababu lipo katikati ya nchi na ndio kitovu…lakini zaidi mama huyu
yupo hapa na kwa maombezi yake anaendelea kuimarisha ulinzi wa taifa letu,”
alisema NdahaniNdahani ambaye
ni miongoni mwa vijana walioshiriki kukimbiza Mwenge wa Uhuru 2017, katika hotuba
yake amemfananisha Rais John Magufuli na Nabii Musa kwa namna anavyoongoza taifa
kwa unyenyekevu na maono ya kimungu huku nchi ikishuhudia miujiza mikubwa katika
kipindi hiki kigumu.Kijana huyo
ambaye amekuwa na juhudi kubwa za kuhamasisha umoja wa kitaifa kupitia vijana
wa mkoa wote wa Singida, amewataka watanzania walionusurika na ugonjwa wa Corona
na wale waliopona kuendelea kuchukua tahadhari zinazoelekezwa na wataalamu na
Rais, ili kuepuka maambukizi mapya.“Kwa wakristu
mkifatilia kitabu kile cha ‘Kutoka’ mtakumbuka namna Mungu alivyomuongoza Musa
katika kuwavusha wana wa Israeli kwenye bahari ya Shamu kwa kutumia ile fimbo…na
ndivyo baba yetu Magufuli anachokifanya kwa sasa,” alisema Ndahani huku akishangiliwaKupitia
maombi hayo ya shukrani, Sista wa Kanisa Katoliki la Moyo Mtakatifu wa Yesu,
Jimbo Katoliki la Singida, Maria Subi, alisema anamshukuru Mungu kwa namna ya
kipekee hasa anavyojidhihirisha katikati ya kiongozi mkuu wa Tanzania Rais
Magufuli, kwa namna anavyoonesha hekima na utulivu mkubwa… wakati wote anaposhughulikia
suala la corona“Kwa nguvu
yake Mwenyezi Mungu furaha na amani ya watanzania imeanza kurejea tena, na
tayari tumeanza kuungana na wageni mbalimbali kwa kuwakaribisha. Naamini sasa tutaendelea
kufanya kazi zetu kama kawaida na nchi itachangamka kama mwanzo, tunapaswa kumshukuru
Mungu” alisema Subi.

Post a Comment

0 Comments