Soka Letu leo Jumanne 12.05.2020: Ozil, Ceballos, Todibo, Gomes, Vinicius, Mahrez

Mesut Ozil (Kushoto) akiwana Kevin de Bruyne wa Manchester City

Mchezaji nyota wa Arsenal Mesut Ozil, 31, hataondoka klabu hiyo msimu huu na badala yake atakamilisha mwaka mmoja uliosalia katika mkataba wake na Gunners . (Fanatik, via Football London)

Arsenal wanamatumaini ya kusalia na kiungo wa kati wa Real Madrid Dani Ceballos, 23, kwa mkopo hadi msimu wa sasa wa ligi ya primia utakapo kamilika, lakini wanapanga kurefusha mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania katika klabu hiyo kwa msimu mwingine. (El Confidencial, via Metro)

Dani CeballosHaki miliki ya pichaEPA
Image captionArsenal wana matumaini ya kusalia na kiungo wa kati wa Real Madrid Dani Ceballos

RB Leipzig wameungana na Everton katika kinyang'anyiro cha kumsaka beki wa Ufaransa wa miaka 20- Jean-Clair Todibo kutoka Barcelona. (HITC)

Manchester United wanataka kumsaini kiungo mahiri wa Argentina Thiago Almada, 19, ambaye pia ananyatiwa na Arsenal, kutoka Velez Sarsfield. (Tutto Mercato Web, via Express)

Manchester United bado hawajakubaliana kuhusu mkataba mpya na kiungo wa kati Angel Gomes,19, ambaye mkataba wake wa sasa unakamilika mwisho wa Juni. (Goal)

Angel Gomes
Image captionManchester United hawajakubaliana na kiungo wa kati Angel Gomes, kuhusu mkataba mpya

Mshambuliaji wa Benfica Carlos Vinicius analengwa na Manchester United, kiungo huyo raia wa Brazil aliye na miaka 25 anaweza kununuliwa na klabu nyingine ikiwa italipa £88m kabla ya kuanza majadiliano ya mkataba. (Sun)

Winga wa Algeria Riyad Mahrez, 29, anasema Liverpool walitaka kumsajili kabla ya ajiunge na Manchester City kutoka Leicester City lakini Reds walisitisha mpango huo walipompata Mohamed Salah kutoka Roma. (Bein Sports, via Manchester Evening News)

Riyad MahrezHaki miliki ya pichaREX FEATURES
Image captionWinga wa Algeria Riyad Mahrez

Chelsea wana amini watampata Charlie Webster, ambaye anaripotiwa kunyatiwa na Borussia Dortmund, katika mkataba wa wa kitaalamu atakapofikisha miaka 17 Januari ijayo. (Telegraph)


ADVERTISEMENT


Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu

Mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, alimuahidi marehemu babu yake kuwa atachezea Real Madrid. (Sun)

Mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick AubameyangHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang

Gunners pia wanakabiliwa na pigo jingine la kumkosa beki wa RB Leipzig wa miaka 21-Mfaransa Dayot Upamecano baada ajenti wake kusema kuwa huenda asihame kutokana na janga la coronavirus. (Sport 1, via Metro)

Shanghai Shenhua inatarajia kuwa mshambuliaji wake Odion Ighalo, 30, raia wa Nigeria atarejea klabu hiyo baada ya kuchezea Manchester United kwa mkopo kabla ya msimu mpya wa ligi kuu ya China, ambayo imepangiwa kuanza mwezi Julai. (Sky Sports)

Shanghai Shenhua inatarajia kuwa mshambuliaji wake Odion Ighalo, 30, atarejea klabu hiyo kutoka Manchester UnitedHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionShanghai Shenhua inatarajia kuwa mshambuliaji wake Odion Ighalo, 30, atarejea klabu hiyo kutoka Manchester United

Tottenham na Arsenal wameongeza juhudi za kumsaka kiungo wa kati wa Brazil Willian kwa sababu mashauriano ya kiungo huyo wa miaka 31 kurefusha mkataba Chelsea yamegonga mwamba. (football.london)

Manchester United wamefufua azama yao ya kumsaka mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, 22. (Sport, via Mail)

ChelseaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWachezaji wa Chelsea wakisherehekea ufungaji bao

Mkufunzi wa Chelsea Frank Lampard ametumia mtandao wa kijamii wa Instagram kumfuatilia Dries Mertens, ripoti zinasema Lampard amewasiliana moja kwa moja na mashambuliaji huyo wa miaka 33- wa Ubelgiji na Napoli. (Express)


ADVERTISEMENT

Post a Comment

0 Comments