tangazo

TAKUKURU yaokoa mil.57 vyama ushirika

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU ,Mkoa wa Morogoro imeokoa sh. milioni 57.8 zilizokuwa mikononi mwa viongozi wa vyama vya ushirika na saccos katika Wilaya za Mvomero na Gairo.

Akitoa taarifakwa waaandishi wa habari, Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Morogoro ,Victor Swella alisema bado watuhumiwa wengine walichota fedha hizo wanaendelea kurejesha ambazo walizifanyia ubadhirifu kinyume na malengo ya vyama vyao.

"Tumeokoa sh. 57,879,725ambazo zilikuwa mikononi kwa viongozi wa vyama vya ushirika saccos kwenye Wilaya ya Mvumerona Gairo," alisema Swella. Alisema katika kipindi hicho , TAKUKURU ilibaini kuwapa kwa wateja sugu wa mamlaka ya maji safu na usafafi wa mazingira Morogoro ,kutolipa madeni yao yaliyotakana na huduma ya majitaka

Wakati huo huo, TAKUKURU Mkoa imetoa wito kwa halmashauri zote zilizopokea michango na misaada kwa ajili ya kujikinga na virusi vya corona itumike kwa lengo lililokusudiwa na haitasita kuwachulia hatua watakahujumu mapambano na kujikinga nacorona.

Pia alitoa wito kwa wananchi wa mkoa huo kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na TAKUKURU katika mapambanodhidi ya rushwa Nchini.

Post a Comment

0 Comments