tangazo

TAKUKURU yawakamata wafanyabiashara 12 kwa kuuza viwatilifu vinavyotolewa kwa mkopo

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Mara (TAKUKURU) imewakamata wafanyabiashara 12 kwa tuhuma za kuuza viwatilifu vyenye nembo ya bodi ya pamba vinavyotolewa kwa kuwakopesha wakulima.

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake Kamanda Mkuu wa TAKUKURU Mkoani humo, Alex Kuhanda amesema kuwa viwatilifu vilivyokutwa madukani vina jumla ya shilingi milioni nane vikiuzwa na wafanyabishara hao kati ya shilingi 6000/- hadi ya 6500/- wakikinzana na bei elekezi ya shilingi elfu 4000/- ambapo mkulima anapata kwa mkopo na hulipa baada ya mavuno.

"Tumefanya uchunguzi wa awali kwenye wilaya za Serengeti, Butiama, Bunda na Musoma vijijini na kubaini wanaopeleka viwatilifu kwenye maduka binafsi ni miongoni mwa wanachama wa AMCOS pamoja na wakala waliopata zabuni ya kusambaza kwa wakulima," amesema Kuhanda.

Aidha kamanda Kuhanda amesema kuwa, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao pindi uchunguzi utakapokamilika na kuwabainisha kuwa wamehusika, ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia za namna hiyo zinazowadidimiza wakulima wa pamba na kuwatengenezea fikra hasi kuwa serikali haiwasaidi
i.

Post a Comment

0 Comments