Tetemeko la ardhi latoke nchini Indonesia na Japan

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5,5 katika kipimo cha Richter laripotiwa kutokea katika eneo la Ibaraki Mashariki mwa Japan na katika mkoa wa Maluku nchini Indonesia.

Nchini Indonesia katika eneo hilo la mkoa wa Maluku, tetemeko lililkuwa na ukubwa wa 5,7 katika kipimo cha Richter.

Kulingana na taarifa ziliztolewa na  kitengo kinachohusika na utafiti wa ardhi na tetemeko nchini Japan, tetemeko hilo lenye ukubwa wa  5,5  limesikika katika umbali wa kilomita 50 na kitovu chake.

Tetemeko hilo limetokea majira ya asubuhi  saa mbili  na kusikika katika maeneo tofauti karibu na eneo la kitovu cha tetemeko.

Kwa upande wake , kitengo cha utafiti kuhusu tetemeko na ardhi nchini Indonesia kimefahamisha kuwa  kitovu cha tetemeko Maluku Tengagara  limesikika katika umbali wa kilomita 10.

Hakuna tahari yeyote iliotolewa kuhusu uwezekano wa kutokea kwa wimbi kubwa la Tsunami.
Watu  36 walifarik katika  tetemeko lililokuwa na ukubwa wa  6,8 lililotokea Septemba  26 mwaka  2019 Maluku.

ADVERTISEMENT

Post a Comment

0 Comments