tangazo

Tetesi za soka leo 29/05/2020

Leicester wamempatia kiungo wa kati wa Liverpool Adam Lallana, ofa ya mkataba wa kudumu. Mkataba wa kiungo huyo wa kimataifa wa England, Anfield unakamilika mwisho wa mwezi Juni. (Football Insider)

Klabu tano za ligi ya Premia - Chelsea, Newcastle, Manchester United, Arsenal na Leicester - zinamtaka kiungo wa kati wa Barcelona na Brazil midfielder Philippe Coutinho. Nyota huyo wa miaka 27, ambaye kwa sasa yuko Bayern Munich kwa mkopo, anatarajiwa kuuzwa kwa karibu £90m. (Mundo Deportivo - in Spanish)


Real Madrid wamepokea ofa kutoka kwa klabu zinazomtaka mshambuliaji wa Wales Gareth Bale,30, lakini mchezaji huyo anatarajiwa kusalia katika klabu hiyo kwa mwaka mwingine mmoja. (Marca)

Manchester United na Newcastle wanamtaka winga wa Uruguay Facundo Pellistri,18, ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Penarol. (Mail)

Galatasaray wanapania kushinda usajili wa winga wa Bournemouth Ryan Fraser. Kiungo huyo Scotland pia ananyatiwa na Arsenal naTottenham. (Daily Record)


Everton itafanya mazungumzo na Djibril Sidibe kuhusu kurefushwa kwa mkopo wake ligi ya Premia itakaporejelewa mwezi Juni. (Liverpool Echo)

Shanghai Shenhua wamelegeza msimamo wao kumruhusu mshambuliaji wa Nigeria Odion Ighalo,30, kurefusha muda wake wa mkopo Manchester United. (ESPN)

Paris St-Germain wanakaribia kuafikiana kuhusu mkataba wa Mario Icardi. Muargentina, huyo wa miaka 27, yupo PSG kwa mkopo kutoka Inter Milanlakini mkataba wake unakamilika Mei 31. (Sky Sports)


PSG pia wanatafakari uwezekano wa kumsajili mchezaji nyota wa Chelsea Willian,31, ambaye huenda akawa tayari kuondoka kwa mkataba wa bila malipo mwisho wa msimu huu. (Le10Sport - in French)

Liverpool huenda wakacheza mechi yao ya nyumbani iliyosalia sehemu itakayokubalika na wote, endapo ligi ya Premia itarejelewa tarehe 17 Juni. (Times - subscription required)

Inter Milan wanatarajiwa kumuongezea mkataba beki wa zamani wa Manchester United Ashley Young ambaye alijiung ana klabu hiyo ya Italia Januari kwa mkataba wa awali wa miezi sita. (Telegraph - subscription required)

Mshambuliaji wa England Jadon Sancho ametatizika na tetesi kwamba anataka kuhama Borussia Dortmund, amesema mchezaji mwenzake Thomas Delaney. Sancho, 19, anahusishwa na uhamisho wa kuenda Manchester United. (ESPN)

Post a Comment

0 Comments