Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 14.05.2020: Werner, Sane, Dembele, Bakayoko, Bellingham, Havertz

Bayern Munich wanatafakari kuwasilisha ofa ya zaidi ya £50m kumsajili winga wa Manchester City Leroy Sane. (Telegraph)
Manchester United wanataka kiungo wa kati wa miaka 16 Jude Bellingham kucheza katika kikosi cha kwanza wakifanikiwa kumsajili kutoka Birmingham City msimu huu. (Evening Standard)
Manchester United imemnunua mshambuliaji wa Ufaransa na Lyon Moussa Dembele,23, ambaye pia analengwa na Chelsea, kwa £61.8m. (Todofichajes, via Express)
Barcelona wameweka dau la £53m dhidi ya mshambuliaji wa Ufaransa wa miaka 22- Ousmane Dembele, ambaye walimsajili kwa mkataba wa £135.5m. (Marca, via Star)
Barcelona wameweka dau la £53m dhidi ya mshambuliaji wa Ufaransa wa miaka 22- Ousmane Dembele,Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBarcelona wameweka dau la £53m dhidi ya mshambuliaji wa Ufaransa wa miaka 22- Ousmane Dembele
Vilevile Barcelona imefanya mazungumzo na Juventus kuhusu usajili wa beki wa Italia Mattia de Sciglio, 27, kutoka upande wa Serie A baada ya mazungumzo ya mkataba na beak wa Portugal Nelson Semedo, 26, kugonga mwamba. (Marca)
Tottenham imetangaza mango wa kumuuza beki wake Juan Foyth na Barcelona wameonesha Ina ya kutaka kumnunua kiungo huyo wa miaka 22-kutoka Argentina. (Mirror)
chelseaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Chelsea wako tayari kumuuza kiungo wa kati Mfaransa Tiemoue Bakayoko, 25, kwa £31m lakini Paris St-Germain hawataki kutumia zaidi ya £26.5m kumsajili. (Le10 Sport, via Star)
Kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen Kai Havertz, 20, amehusishwa na totes za kujiunga na Chelsea, Liverpool na Manchester United lakini mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani Michael Ballack ameshauri asiondoke Katina klabu yake ya sasa. (Football London)
kipa wa Everton Mholanzi Maarten Stekelenburg,Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKipa wa Everton Mholanzi Maarten Stekelenburg
Everton wanajiandaa kumuachia kipa wao Mholanzi Maarten Stekelenburg, 37, kuondoka katana wake ukimalizika mwisho wa msimu huu ili kumtafuta kipa mwengine.

Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 13.05.2020

mshambuliaji wa Real Madrid forward Gareth Bale
Newcastle wako tayari kutumia £53m kumpata mshambuliaji wa Real Madrid, Gareth Bale, 30, mpango ambao ukifanikiwa utamrejesha ntota huyo katika ligi kuu ya England msimu huu. (Daily Mail)
Tottenham haitakubali Tanguy Ndombele, 23, kuondoka klabu hiyo msimu huu. Kiungo huyo wa kati wa Mfaransa amehusishwa na tetesi za kujiunga na Barcelona na Liverpool. (Independent)
Dejan Lovren anakaribia kuondoka Liverpool, huku Roma ikitarajiwa kuwasilisha ofa ya kumnunua beki huyo wa Croatia wa miaka 30. (Gazzetta dello Sport, via Liverpool Echo)
Liverpool imeungana na miamba wengine wa Ulaya kumsaka kiungo wa kati wa Red Bull Salzburg na Hungary Dominik Szoboszlai,19. (Tuttosport, via Daily Mail)
SanchoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Manchester United wanataka kuwasajili wachezaji watatu wa Uingereza msimu huu akiwamo- mshambuliaji wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 20, kiungo wa kati wa Aston Villa Jack Grealish, 24, na kiungo wa kati wa Birmingham wa miaka 16, Jude Bellingham. (Daily Star)
Hata hivyo huenda, mshambuliaji Odion Ighalo, 30, akacheza mechi yake ya mwisho Manchester United maada y amazungumzo ya kurefusha makataba wa mkopo wa kiungo huyo wa kimataifa wa Nigeria kutoka Shanghai Shenhua nchini China kugonga mwamba. (Standard)
Paul PogbaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Juventus wamekuwa klabu ya kwanza ya Italia kuweka kanuni ya mshahara kwa wachezaji wake, hatua ambayo imewafanya kujiondoa katika kinyang'anyiro cha kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba,27 . (Daily Mail)
Lionel Messi, 32, na baadhi ya wachezaji wenzake nchini Uhispania huenda wakapunguziwa mshahara kwa asilimia 30 msimu ujao huku Barcelona na Real Madrid wakitathmini hatua ya kupunguza marupurupu ya wachezaji kutokana na athari iliyosababishwa na virusi vya corona. (Sun)
Angel GomesHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Chelsea wana uhakika wa kumsajili kiungo wa Manchester United, Angel Gomes mwenye umri wa miaka 19. (Mirror)
West Brom itachuana na Tottenham kumsajili mshambuliaji wa Fenerbahce na Kosovo Vedat Muriqi, 26, mwenye thamani ya £uro milioni 18 iwapo atafanikiwa kupanda daraja. (Aksam, via Birmingham Mail)
Crystal Palace inamtaka bosi wa Burnley Sean Dyche kuwa meneja wao. (Mirror)

Post a Comment

0 Comments