tangazo

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 01.05.2020: Grealish, Sancho, Fekir, Coutinho, Moses, Semedo

Real Madrid na Barcelona wamejiunga na kinyang'anyiro cha kumsajili winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho. Manchester United pia wako mbioni kumsaka nyota huyo wa miaka 20-year-old. (Bild - in German)
Manchester United inapigiwa upatu kumnunu kiungo wa kati wa Aston Villa midfielder Jack Grealish, 24, kuliko mchezaji mwenza wa England na Leicester James Maddison, 23. (Manchester Evening News)
Arsenal inakabiliwa na ushindani kutoka kwa AC Milan kumsajili kiungo wa kati wa Real Betis na Ufaransa Nabil Fekir, 26. (Marca - in Spanish)
Nabil FekirHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionArsenal inakabiliwa na ushindani kutoka kwa AC Milan kumsajili kiungo wa kati wa Real Betis Nabil Fekir
Bayern Munich wako tayari kulipa £60m tu kumnunua winga wa Manchester City na Ujerumani Leroy Sane, 24. (Sky Sports)
Barcelona haitamuuza winga wa Brazil Philippe Coutinho kwa bei ya chini ya euro milioni 100 sawa na (£87m). Chelsea wamehusishwa na kiungo huyo matata wa miaka 27. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Philippe CoutinhoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBarcelona haitamuuza winga wa Brazil Philippe Coutinho kwa bei ya chini ya euro milioni 100
Inter Milan wako tayari kubadilisha mkataba wa Victor Moses wa mkopo kuwa wa kudumu lakini wanataka Chelsea isitishe na mpango kutaka kumuuza winga huyo wa Nigeria wa miaka 29. (Calciomercato)
Manchester City wameanza kujadiliana na Barcelona kumhusu beki wa Portugal Nelson Semedo, 26. Mkataba huo utamjumuisha beki mwezake wa Portugal Joao Cancelo, 25, kujiunga na upande mwingine. (Sport)
Victor MosesHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionInter Milan wako tayari kumpatia mkataba wa kudumu winga wa Chelsea Victor Moses
Kiungo wa kati wa Brazil Fernandinho, 34, anataka kusaini mkataba mpya Manchester City. (Sky Sports)
Winga wa Bournemouth na Scotland Ryan Fraser, 26, anataka kujiunga na Tottenham mkataba wake utakapomalizika msimu huu. (Football Insider)
Manchester United huenda isikubali ofa yoyote ya kumuuza kipa wake Dean Henderson, 23, dirisha la uhamisho litakapofunguliwa. Kipa huyo Muingereza kwa sasa yuko Sheffield United. (ESPN)
Dean HendersonHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionManchester United haina mpango wa kumuuza kipa wake Dean Henderson
Mshambuliaji wa Aston Villa Mhispania Borja Baston, atarejea katika klabu yake ya zamani Real Zaragoza mkataba wake utakapomalizika msimu huu. Kiungo huyo wa miaka 27- alijiunga na Villa mwezi Januari. (Sport Aragon - in Spanish)

Tetesi za Soka Alhamisi

Arsenal wameripotiwa kuwasiliana na Real Madrid kuhusu uhamisho wa beki wa Uhispania Sergio Reguilon, 23, ambaye yupo Sevilla kwa mkopo. (ABC, via Star)
Sergio ReguilonHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMchezaji matata wa Real madrid anayesakwa na Arsenal
Mauricio Pochettino ni chaguo la kwanza la mmiliki mtarajiwa wa Newcastle kuchukuwa nafasi ya mkufunzi Steve Bruce na wako tayari kumlipa £19m kwa mwaka. (Sky Sports)
Mkufunzi wa Bayern Munich Hansi Flick amefanya mazungumzo ya simu ya dakika 30 na winga wa Manchester City na Ujerumani Leroy Sane, 24, kujadili uwezekano wa uhamisho wake. (Bild, via Goal - in German)
Leroy Sane
Arsenal wameambiwa lazima walipe zaidi ya £25m ikiwa wanataka kumnunua mshambuliaji wa Celtic na Ufaransa Odsonne Edouard, 22. (Express)
Mshambuliaji wa Napoli Dries Mertens, 32, anataka kuhamia London, huku Chelsea ikiwa bado inamnyatia kiungo huyo wa kimataifa wa Ubelgiji. (Mail)
Kiungo wa Ufaransa Tanguy Ndombele, 23, anatathmini hatima yake ya baadae katika klabu ya Tottenham, huku Barcelona wakimmezea mate. (Sky Sports)

Post a Comment

0 Comments