Tetesi za soka Ulaya Jumamosi tarehe 09.05.2020 : Victor ,Savic, Pjanic, Eriksen, Umtiti

Manchester wana wasiwasi kumuhusu Victor Lindelof

Mashaka juu ya uwezo wa Victor Lindelof yamesababisha Manchester United kuwa na nia ya kujiimarisha katika safu ya ulinzi wa kati. (ESPN)

Manchester United wanatafakari juu ya beki wa kati wa Real -Valladolid wa Ghana mwenye umri wa miaka 21, Mohammed Salisu, na klabu hiyo inataka kusaini ya beki huyo Mghana msimu ujao ilikumpa Victor Lindelof ushindani zaidi. (ESPN)

Liverpool wanayo hamu ya kumsaini mshambuliaji wa Mbrazil Talles Magno,Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionLiverpool wanayo hamu ya kumsaini mshambuliaji wa Mbrazil Talles Magno,

Sergej Milinkovic-Savic anaweza kuondoka Lazio msimu huu na Manchester United wapo tayari kumchukua Mserbia huyo mwenye umri wa miaka 25 ikiwa atafanya hivyo. (Star)

Liverpool wanayo hamu ya kumsaini mshambuliaji wa Mbrazil Talles Magno, 17, kutoka Vasco da Gama ya Brazil, na Benfica, Lyon na Sevilla pia wako kwenye mbio za kutaka kunasa saini ya mchezo huyo. (Express via AS)

Kiungo wa kimataifa wa Juventus Bosnia Miralem Pjanic, 30, amekubali kujiunga na Barcelona msimu ujao. (Gazetta dello Sport)

'Bosnia Miralem Pjanic, 30, amekubali kujiunga na Barcelona msimu ujao
Image captionBosnia Miralem Pjanic, 30, amekubali kujiunga na Barcelona msimu ujao

Barcelona wanapambana kupata saini ya mshambuliaji wa Argentina na Inter Milan Lautaro Martinez, 22, na wametoa chaguo la wachezaji sita, pamoja na beki wa katikati mwenye umri wa miaka 26 Samuel Umtiti, kama sehemu ya mpango wa kubadilishana. (Sport - in Spanish)

Christian Milik's Eriksen, 28, amelazimika kuishi katika uwanja wa mazoezi wa kilabu kipindi hiki ambacho watu wamefungiwa ndani, na kiungo huyo wa Denmark bado hajapata nyumba tangu ahamie Januari kutoka Tottenham. (Sun)

Mshambuliaji wa Argentina na Inter Milan Lautaro MartinezHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMshambuliaji wa Argentina na Inter Milan Lautaro Martinez

Nia ya Real Madrid kwa kiungo wa Rennes Angolan Eduardo Camavinga, 17, unashikiliwa na janga la homa kali ya mapafu.(Marca)

West Ham itamruhusu kiungo wa Uingereza Nathan Holland, 21, kuondoka kwa kitita cha pauni milioni moja msimu ujao, na Sheffield Wednesday waonyesha nia. (Football Insider)

Arsenal wanataka kusaini beki wa Leicester na Uholanzi mwenye umri chini ya miaka 19 kamili Dennis Gyamfi, 18. (Football Insider)

Samuel Umtiti miongoni mwa wachezaji wanaosakwa na BarcelonaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSamuel Umtiti miongoni mwa wachezaji wanaosakwa na Barcelona

Washika mitutu wa London wako kwenye mazungumzo ya kumsaini mshambuliaji wa pembeni kutoka Norway mwenye miaka 19 George Lewis, kwasasa ni mchezaji huru, baada ya kushawishi viongozi wa kilabu hicho. (Football London)

Klabu ya Ufaransa Lyon imedhamiria kuimarisha safu yake ya ulinzi majira ya joto na wanamipango tayari na mabeki wa nne.(L'Equipe)

Tetesi bora za Ijumaa tarehe 08.05.2020:

Philippe Coutinho ameshindwa kutamba Barcelona na amepelekwa Bayern kwa mkopoHaki miliki ya pichaQUALITY SPORT IMAGES/GETTY
Image captionPhilippe Coutinho ameshindwa kutamba Barcelona na amepelekwa Bayern kwa mkopo

Klabu ya Newcastle itatumia pauni milioni 70 kumsajili mchezaji wa nafasi ya kiungo wa Barcelona, raia wa Brazil Philippe Coutinho ikiwa pendekezo la klabu hiyo kununuliwa litafanikiwa. Mchezaji huyo mwenye miaka 27 anaichezea Bayern Munich kwa mkopo. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Kampuni ambayo inaelekea kuwa wamiliki wapya wa Newcastle pia inataka kumsajili beki wa kati wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, 28. Mchezaji huyo anatarajiwa kuondoka kwenye klabu hiyo ya Italia kwa kitita cha pauni milioni 69.8. (Sky Sports via Star)

Klabu ya Newcastle itatumia pauni milioni 70 kumsajili mchezaji wa nafasi ya kiungo wa Barcelona, raia wa Brazil Philippe Coutinho ikiwa pendekezo la klabu hiyo kununuliwa litafanikiwa. Mchezaji huyo mwenye miaka 27 anaichezea Bayern Munich kwa mkopo. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Kampuni ambayo inaelekea kuwa wamiliki wapya wa Newcastle pia inataka kumsajili beki wa kati wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, 28. Mchezaji huyo anatarajiwa kuondoka kwenye klabu hiyo ya Italia kwa kitita cha pauni milioni 69.8. (Sky Sports via Star)

Arsenal wanaweza kupewa nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa Inter Milan Mauro Icardi, 27, ikiwa ni mbadala wa mshambuliaji Pierre- Emerick Aubameyang, 30. Mkataba wa Aubameyang unatarajiwa kumalizika msimu ujao, wakati Icardi anacheza kwa mkopo Paris St-Germain. (Tuttosport via Teamtalk

Washika bunduki hao pia wako njiani kuingia makubaliano na mchezaji huru George Lewis. Winga huyo wa Norway mwenye miaka 19, alikuwa akiichezea Tromso. (Metro via Goal)

Sergej Milinkovic-Savic (kulia) anayenganganiwa na timu kadhaaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSergej Milinkovic-Savic (kulia) anayenganganiwa na timu kadhaa

Mchezaji wa miaka 16, wa klabu ya Barcelona Marc Jurado ametupilia mbali ofa kuchezea klabu hiyo ya Uhispania. Beki huyo wa kulia anajiandaa kujiunga na Manchester United.(ESPN)

Unaweza pia kutazama:

Muamuzi wa soka wa Tanzania anayefanyia mazoezi sebuleni

Post a Comment

0 Comments