tangazo

Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 6.5.2020: Pogba, Ramsey, Fernandes, Pepe, Mbappe, Willian, Chiesa

Aaron Ramsey alifunga bao lake la nne kwa Juventus na kuishinda Inter Milan
Manchester United wako makini kumsajili kiungo wa kati wa Juventus na Wales Aaron Ramsey, 29, kama sehemu ya makubaliano ya mabadilishano na mchezaji wa Ufaransa Paul Pogba, 27. (Express)
Sporting Lisbon imeripotiwa kwa Fifa na Sampdoria, inayodai kwamba inawadai euro milioni 4 baada ya kumuuza Bruno Fernandes, 25, kwa Manchester United Januari. Mchezaji huyo kiungo wa kati raia wa Ureno alitoka Italia na kwenda Sporting 2017. (Mirror)
Nicolas PepeHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionArsenal ilimsajili winga Nicolas Pepe mchezaji wa Ivory Coast Nicolas Pepe kutoka Lille kwa kima cha £72m.
Arsenal huenda ikalazimika kuuza wachezaji wake sita ili kupata pesa za kulipa pesa zilizosalia kwa winga wa Ivory Coast Nicolas Pepe euro milioni 72 kwa hatua yake ya kutoka Lille msimu uliopita. (Sun)
Winga wa Chelsea Willian, 31, anatarajiwa kusalia London mkataba wake Stamford Bridge utakapofikia ukomo Juni, huku mchezaji huyo wa Brazil akitarajia kuungana na kocha wake wa zamani Jose Mourinho at Tottenham. (Mail)
Federico Chiesa celebrates his hat-trick for FiorentinaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionFederico Chiesa mchezaji wa Fiorentina
Juventus itaendelea na azma yake ya kumwinda winga wa Italia Fiorentina Federico Chiesa, wakati ambapo klabu yake iko tayari kumuuza kwa tahamani yake anastahili huku Chelsea, Manchester United pamoja na Inter Milan pia nao wakiwa wanammezea mate mchezaji huyo, 22. (Goal)
Manchester City wameonesha nia ya kumsajili Lucas Martinez, 23, wa River Plate Quarta, na wanataka raia huyo wa Argentina kujumuika na wachezaji kuijiunga na Manchester City katika wanja wa Etihad huku mlinzi mwenzake Nicolas Otamendi, 32, akielekea kwengineko. (Sports Witness via TNT Sports - in Spanish)
Sheffield United goalkeeper Dean HendersonHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionDean Henderson ameshiriki kila mechi katika msimu huu wa Ligi ya Primia
Manchester United inahitajika kufanya maamuzi juu ya hatma ya mlinda lango Muingereza wa Under-21 Dean Henderson, 23, ambaye ameonesha umahiri wake wakati akiwa Sheffield United kwa mkopo, ikizangatiwa kwamba mkataba wake unamalizika mwisho wa Juni. (Sun)
Matumaini ya Everton kumsajili mchezaji wa Napoli Allan, 29, yanadidimia wakati ambapo mmiliki wa klabu hiyo ya Serie A akisema thamani ya kiungo wa kati wa Brazil ya euro milioni 65 ikitarajiwa kupungua kwasababu ya Covid-19 - sawa na ilivyo kwa mchezaji mlinzi wa Senegali Kalidou Koulibaly, 28, anayelengwa na Liverpool anayesemekana kuwa na thamani ya euro milioni 95. (Il Napolista - in Italian)
Kylian MbappeHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionHadi kufikia Machi 4, 2020, Kylian Mbappe alikuwa amefunga magoli sita katika michezo mitatu iliyotangulia aliyocheza kwa Paris St-Germain
Msambulizi wa Paris St-Germain na Ufaransa Kylian Mbappe, 21, ameomba kuruhusiwa kuhama timu hiyo kwenda Real Madrid au klabu nyengine yoyote ya Ulaya siku za usoni. (AS - in Spanish)
Arsenal inataka kumsaka kiungo wakati wa Bayern Munich Angelo Stiller, 19. (Bild - in German)
Mshambuliaji wa Juventus na Argentina Gonzalo Higuain bado hajaamua ikiwa atarejea Italia kutoka kwao huku klabu yake ya tangu utotoni River Plate ikitaka kumsajili mhcezaji huyo, 32. (TuttoSport - in Italian)

Post a Comment

0 Comments