tangazo

Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 25.5.2020: Coutinho, Aubameyang, Higuain, Jimenez, Dembele

Arsenal inatarajiwa kuanza mazungumzo na wakala wa kiungo wa kati wa Barcelona Phillipe Coutinho.
Mchezaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 27 amehudumia msimu wote akiwa kwa mkopo katika mabingwa hao wa Ujerumani Bayern Munich, lakini klabu hiyo haiko tayari kulipa paundi milioni 105 za Uingereza ili kufanikisha mkataba wa kudumu.(Le10sport - in French)
Paris St-Germain inafanya mazungumzo na Arsenal katika jaribio la kumsaini mashambuliaji wa klabu hiyo Pierre-Emerick Aubameyang, 30, for £34m. (Todofichajes)

Pierre-Emerick AubameyangHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang

Mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 32, huenda akarudi katika ligi ya premia baada ya uhamisho wake wa mkopo katika klabu ya Chelsea - Newcastle na Wolves zote zinamwania. (Express)
Mshambuliaji wa klabu ya RB Leipzig Timo Werner, 24, amehusishwa pakubwa na uhamisho wa kujiunga na Liverpool lakini aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Manchester United Owen Hargreaves anahisi kwamba uhamisho wa klabu hiyo ya Old Trafford ungekuwa bora zaidi kwa mchezaji huyo. (Star)
Mshambuliaji wa Wolves Raul Jimenez, 29 mwenye thamani ya £57m, ananyatiwa na Manchester United, Arsenal na Real Madrid. (Tuttosport - in Italian)

Raul JimenezHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMshambuliaji wa Wolves Raul Jimenez(Kulia) ananyatiwa na Manchester United

Mshambuliaji wa Bournemouth Joshua King, 28, analengwa na klabu sita zilizopo katika uongozi wa ligi ya Premia baada ya ombi la dau la paundi millioni 20 katika siku ya mwisho ya uhamisho kukataliwa mnamo mwezi Januari. (Mirror)
Juventus inataka kuipiku Real Madrid katika ununuzi wa mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, 19, katika uhamisho wa dau la £67m. (Tuttosport - in Italian)
Barcelona iko tayari kumuuza mashambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele, 23, kwa dau la £37m. Klabu hiyo ya Uhispania ililipa £137m kumnunua raia huyo wa Ufaransa miaka mitatu iliopita lakini ameanzishwa mara tano pekee kufuatia msururu wa majeraha. (Mirror)

Barcelona iko tayari kumuuza mashambuliaji wa Ufaransa Ousmane DembeleHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBarcelona iko tayari kumuuza mashambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele

Winga Adama Traore, 24, ameshauriwa kuipuuza hamu ya Liverpool na kusalia katika klabu ya Wolves kwa msimu mwengine na mchezaji wa zamani wa Sheffield United Michael Brown. (Star)
Winga wa Wales na klabu ya FC Schalke Rabbi Matondo, 19, anasema kwamba amejiandaa vilivyo kujiunga na klabu hiyo ya Ujerumani huku kukiwa na hamu kutoka kwa Manchester United. (Manchester Evening News)

Tetesi za Soka Jumapili

Wakala wa Paul Pogba Mino Raiola ameanza mazungumzo na Juventus kuhusu uhamisho, lakini Real Madrid na Paris St-Germain pia wanamtolea macho kiungo huyo wa Machester United, 27. (Le10sport - in French)

Paul PogbaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Bayern Munich inaweza kuingilia mipango ya kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer kumsajili winga wa Borussia Dortmund Jadon Snacho, 20. (Sun)
Barcelona wako tayari kuwauza wachezaji wao sita msimu huu wakati huu ambapo hali ya kifedha katika klabu hiyo ni mbaya kwasababu ya virusi vya corona. (Marca)
Manchester United sasa wanapenda kumsajili beki wa kati wa Napoli Kadou Koulibaly, 28, baada ya PSG,Barcelona na Real Madrid kujiondoa kwenye mbio za kumnasa mchezaji huyo. (Sun)

Kadou KoulibalyHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBeki wa kimataifa wa Senegal, Kadou Koulibaly

Kiungo wa kati wa Chelsea Willian, 31, anasema kuwa kukataa kwa klabu yake kumpa mkataba wa miaka mitatu zaidi kumemfanya kuwa katika mazingira ''magumu''. (Esporte Interativo, via Metro)

Post a Comment

0 Comments