Trump: Hatutafunga shughuli za kawaida tena

Rais Donald Trump akishikilia barakoa yakeholds wakati akiongea katika Ciara yake ya kiwanda cha Ford kilichoko Rawsonville ambacho kimebadilishwa na sasa kinazalisha vifaa vya matibabu, Alhamisi, Mei 21, 2020, (AP Photo…

Rais wa Marekani Donald Trump, amesema kwamba shughuli za kawaida hazitafungwa na watu kutakiwa kukaa nyumbani kwa mara ya pili, hata kama kuna mlipuko mpya wa maambukizi ya virusi vya Corona.
Trump alisema hayo wakati wa ziara yake katika kiwanda cha kutengeneza magari cha Ford, katika jimbo la Michigan, ambacho sasa kinatengeneza vifaa maalum vinavyowasaidia wagonjwa kupumua.
Amesema kwamba magavana wataendelea kufungua majimbo kutokana na shinikizo kutoka kwa raia.
"Nadhani idadi kubwa ya majimbo ambayo bado yana masharti magumu ya kutofungua shughuli za kawaida, yataondoa masharti hayo. Sidhani kwamba watu wataendelea kuvumilia. Hii ni nchi ambayo ni lazima ifungue shughuli za kawaida na tumefanya jambo lililo sawa. Tumeokoa Maisha ya mamilioni ya watu” amesema rais Trump
Rais Trump aliulizwa kuhusu uwezekano wa kutokea maambukizi mapya ya virusi vya Corona baada ya kufungua shughuli za kawaida.
Amesema kwamba hilo linaweza kutokea lakini hiyo sio sababu ya kufunga shughuli za kawaida kwa mara ya pili.

Post a Comment

0 Comments