tangazo

Twitter yamuonya rais Donald Trump dhidi ya kuchapisha ujumbe wa 'uongo'

Donald Trump ameilaumu Twitter kwa kuingilia uchaguzi wa urais wa Marekani wa 2020

Chapisho la rais Donald Trump katika mtandao wa Twitter kwa mara ya kwanza limepatiwa onyo na mtandao huo.
Rais Trump alituma ujumbe uliosema: Haiwezekani kwamba makaratasi ya kupigia kura yaliotumwa kwa njia ya posta yanaweza kukosa kufanyiwa udanganyifu.
Twitter iliweka onyo chini ya chapisho hilo na kutuma ujumbe wake kuhusu habari zinazopotosha.
Bwana Trump alijibu kwa kusema kwamba kampuni hiyo ya mtandao inakandamiza uhuru wa kujieleza.
Onyo hilo la Twitter liliandikwa kwa wino wa buluu na alama ya mshangao chini yake, likipendekeza kwamba wasomaji wanapaswa kuangalia ukweli kuhusu makaratasi ya kupigia kura yanayotumwa kupitia huduma ya posta.

Je Twitter inasema nini kuhusu chapisho hilo la Trump?

Donald Trump's tweet and Twitter's warning sign below the postHaki miliki ya pichaTWITTER
Presentational white space
Kiunganishi hicho cha Twitter kinawaelekeza wasomaji kwenye ukurusa ambao unadai kwamba madai hayo ya rais Trump hayana ushahidi.
Kampuni hiyo ya mtandao ilinukuu vyombo vya habari vya CNN , Washington Post na vingine.
Maelezo hayo yanafuatiwa na kichwa cha taarifa: Kile unachohitaji kujua, ambapo Twitter inarekebisha kile inachosema ni madai ya uongo yaliowasilishwa na rais Trump.
Kampuni hiyo ya mtandao ilikuwa imeahidi kuongeza machapisho kama hayo yenye onyo katika habari inayopotosha ama yenye uongo katika tovuti yake - lakini imechelewa kuchukua hatua dhidi ya rais huyo wa Maarekani.
Twitter iliboresha sera yake kuhusu machapisho yenye onyo mapema mwezi huu.

Je rais Trump amesema nini?

Katika machapisho yake mapya katika mtandao huo, bwana Trump aliishutumu Twitter kwa kuingilia uchaguzi huo wa Marekani unaotarajiwa tarehe 3 novemba 2020.
Alisema kwamba kampuni hiyo ya mtandao wa kijamii ilikuwa inakandamiza uhuru wa kujieleza na mimi kama rais sitakubali hayo kufanyika.
Meneja wa kampeni ya rais Trump Brad Parscale pia aliikosoa Twitter.
''Ushirikiano wa watu wanaoegemea upande mmoja kuthibitisha habari fulani ni mbinu za wazi za kisiasa za Twitter kuonesha upendeleo fulani. Kuna sababu kubwa ni kwa nini tuliondoa matangazo yetu yote katika mtandao huo mwezi mmoja uliopita, na upendeleo wa kisiasa ni mojwapo ya sababu hizo'', alisema bwana Parscale.

Huo ndio mitihani wa kwanza wa Twitter

Uchanganuzi uliofanywa na mwanahabari wa teknolojia wa BBC Zoe Thomas
Hii ikimaanisha kwamba huo ndio mtihani wake wa kwanza kuhusu sheria zake mpya.
Presentational grey line

Uchambuzi

Rais Trump ametumia Twitter kama jukwaa la kukabiliana na wanasiasa wengine pamoja na watu maarufu.
Na sasa huenda ametangaza vita dhidi ya mtandao huo.
Kufuatia uamuzi wa mtandao huo wa kusema kwamba habari hiyo ya Trump ilikuwa inapotosha , alisema katika Twitter kampuni hiyo inakandamiza uhuru wa kujielezea na yeye hatokubali hilo kuendelea.
lakini Twitter kama kampuni nyingine yoyote ya binafsi hujitengenezea sheria kwa yale yote yanayotokea katika jukwaa lake.
Tatizo kubwa kwa wengi ni kwamba hadi siku ya Jumanne , kampuni hiyo haikuonekana kutekeleza sheria zake dhidi ya rais huyo ama viongozi wengine wakuu duniani.
Hii si mara ya kwanza kwa rais Trump kuzua madai kama hayo katika Twitter ambayo baadhi ya watu wanasema yangesababisha wao kufungiwa iwapo wangekuwa ni watu wa hadhi ya chini.
Lakini matamshi makali ya Trump ni miongoni mwa sababu zinazowavutia wafuasi wake walio zaidi ya milioni 80 katika mtandao huo. Kampuni hiyo haingependelea kuwapoteza wafuasi hao.
Inachukulia mbinu hiyo mpya ya kutoa onyo kama njia ya kujaribu kupima hamu ya kuwaruhusu watumiaji wa huduma hiyo ikiwemo rais huyo kusema kile wanochotaka , huku pia ikiwapatia wasomaji wake kinga dhidi ya madai yanayopotosha.
Mkakati huo ulifanikiwa sana kuhusu ujumbe wa Covid-19.
Presentational grey line
Je makaratasi haya ya kupigia kura ni yapi?
Ni makaratasi ya kupigia kura ambayo husambazwa kwa njia ya posta na kurudishwa kwa kutumia sanduku la posta.
Katika kura ya maoni iliyofanywa na kituo cha utafiti cha Pew, asilimia 66 ya Wamarekani walisema kwamba wasingependelea kupiga kura wakati huu wa virusi vya corona.
Wasiwasi kama huo umeongezeka ili kuongeza idadi ya makaratasi ya kura yanayotumwa kupitia masanduku ya posta kwa lengo la kupunguza hatari ya maambukizi.
A mail-in ballot in California. File photoHaki miliki ya pichaREUTERS
Huku kila jimbo likiwa na mbinu ya kupiga kura ya mashambani, mahitaji yake kwa mtu kufuzu yana tofauti kubwa.
Majimbo matano Magharibi mwa Marekani , ikiwemo Washington , Oregon na Colorado, hufanya uchaguzi wake kupitia makaratasi ya kupigia kura yanayotumwa kwa njia ya posta.
Majimbo mengine Kama vile Carlifornia , humpatia mtu yeyote fursa ya kushiriki katika uchaguzi kupitia makaratsi hayo iwapo anataka.
Upande mwIngine majimbo 17 huwataka raia wake kutoa sababu mwafaka , kwa nini wasingependelea kupiga kura binafsi ili kuweza kushiriki uchaguzi huo kupitia njia hiyo ya posta.

Twitter imekataa kuondoa 'uongo unaotisha'

Hatua hiyo inajiri baada ya twitter kutoondoa chapisho la Trump kuhusu kifo cha Lori Klausitis 2001.
Rais huyo alichapisha ujumbe kadhaa akikuza dhana kwamba bi Klausutis aliuawa na mtangazaji wa MSNBC Joe Scarborough.
Mjane wake Timothy Klausutis aliiomba Twitter kuondoa chapisho hilo , akisema lilikuwa na 'uongo wa kutisha'.
Kampuni hiyo ilikataa kuondoa ujumbe huo lakini ikamwambia bwana Klausutis kwamba iliomba msamaha kuhusu uchungu uliosababishwa na taarifa ya rais huyo.

Post a Comment

0 Comments