tangazo

Twitter yazuia ujumbe wa Trump saa chache baada ya kusaini amri ya kudhibiti mitando ya kijamii

Mtandao wa Twitter umeficha ujumbe wa rais Donald Trump katika wasifu wake, na kusema kwamba unakiuka sheria ya kutosifia ghasia.
Na badala ya kufutwa, ujumbe huo umebadilishwa kwa onyo lililoandikwa na unaweza kuonekana kwa kuubofya.
Onyo hilo linasema "Twitter imebaini kwamba huenda kwa maslahi ya umma ujumbe huo ukaendelea kuwepo
Hiyo ni hatua ya hivi karibuni ya mzozo kati ya mtandao wa Twitter na Ikulu ya Marekani.
Bwana Trump aliandika ujumbe kuhusu mji wa Minneapolis, Marekani ambao umekubwa na maandano kwa siku kadhaa baada ya kifo cha mwanaume mweusi aliyekuwa kizuizini.
Twitter screengrabHaki miliki ya pichaTWITTER
Image captionWatumiaji wanahitajika kubofya kitufe cha View yaani 'kutazama' ili kuona ujumbe wa rais
Rais amesema atatuma "jeshi la Taifa", na kufuatia ujumbe huo kwa onyo kwamba "uporaji ukianza, ufyatuaji wa risasi unaanza."
Ujumbe huo wa pili ulifichwa na mtandao wa Twitter kwa kuchochea ghasia.
Sera ya Twitter ya kuongeza onyo badala ya kufuta kabisa ujumbe ambao unavunja sheria zake linapokuja suala la umma ilitangazwa katikati ya 2019. Lakini hakuna mtandao wa kijamii ambao umewahi kutumia sera hiyo dhidi ya bwana Trump - au kuondoa kufuta kabisa ujmbe wake wowote.
"Hii ni hatua ya kishujaa na yenye changamoto zake ambayo haijawahi kuchukuliwa na Twitter - au mtandao wowote wa kijamii," amesema Carl Miller, wa Kituo cha Takwimu cha Mitandao ya Kijamii Uingereza.
"Hatua hii imeendelea kuzua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii kati ya kuhusu suala la matumizi mabaya ya mtandao na uhuru wa kujieleza. Sera ya maudhui mtandaoni haijapata cheche za maneno kama kwa hili."
Presentational grey line
Uchambuzi na Rory Cellan-Jones, mwanahabari wa masuala ya teknolojia
Kwa miaka minne mtandao wa Twitter ulivumilia wito wa kumchukulia Donald Trump kama mtumiaji mwengine yeyote na kumfanya atekeleze masharti yaliyowekwa. Na Jumatano ikachukua hatua kidogo tu sio kuondoka ujumbe wake lakini kuongeza kiunganishi cha kutathmini ukweli.
Kampuni hiyo ilikuwa na machaguo mawili - kujikunyata au kuendelea kuchukua hatua kulingana na sheria za mtandao huo. Na kwa sasa hivi imechagua kuchukua hatua na kutoa wito kwa rais wa kuacha kuchochea ghasia.
Kwa mtumiaji mwengine yoyote katika hali ya kawaida, ujumbe wake ungekuwa umeondolewa kabisa na pengine hata akaunti yake kufungiwa kabisa.
Na kwasasa hivi inaonekana kana kwamba hakuna njia rahisi kwa pande hizo mbili hasimu - mgogoro mkubwa unanukia juu ya kiwango cha uhuru wa kujieleza na haki za mitandao ya kijamii kupunguza makali ya maudhui yanayotumwa.
Presentational grey line
Hatua hiyo inamaanisha kwamba hakuna mtumiaji mwengine atakayeweza kupenda, kujibu au kuutuma tena ujumbe wa Trump, Twitter imesema - lakini bado mtu anaweza kutuma tena maoni ya kwenye ujumbe huo.
Twitter imesema: "Ujumbe huu unakiuka sera yetu inayohusia na kuchochea ghasia kwa kuzingaia mstari wa mwisho wa ujumbe huo, unaohusisha ghasia, na hatari ya kuchochea hatua kama hiyo kuendelea kuchukuliwa."
"Tumechukua hatua kuzuia wengine ambao huenda wakachochewa kutekeleza vitendo vya ghasia, lakini ujumbe huo umeendelea kuwepo kwasababu ni muhimu kwa umma kuona ujumbe huo kwa kuzingatia kile kinachoendelea kwa manufaa ya umma."
Saa kadhaa baada ya oyno hilo kutolewa, rais Trump alituma ujumbe: "Twitter haifanyi chochote zaidi ya uwongo na propaganda za China au chama cha mrengo wa shoto cha Democrat "
Moja kwa moja alirejelelea hatua ya kutia saini agizo la raisi kwa lengo la kuondoa baadhi ya sheria zinazolinda mitandao ya kijamii.
Je rais wa Marekani amesaini nini?
President Donald TrumpHaki miliki ya pichaAFP
Trump ameamua kuweka saini ya kuondoa baadhi ya marufuku ya kisheria ambayo mitandao ya kijamii inayo.
Saini hiyo inampa mamlaka ya kuweka hatua za kisheria dhidi ya makampuni ya mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter katika sheria walizoweka katika maudhui wanayochapisha katika mitandao yao.
Rais Trump ameishutumu mitandao ya kijamii kwa kushindwa kuwa makini wakati wa kusaini mamlaka ambayo iko huru kuondolewa wakati wa kuweka saini.
Amri hiyo inatarajiwa kukabiliwa na changamoto za kisheria.
Wataalamu wa kisheria wanasema kuwa bunge la Marekani au mfumo wa mahakama lazima iusike ili kubadili sheria iliyopo sasa ambayo inaeleweka kuwa inalinda mitandao ya kijamii.
Rais wa Marekani Donald Trump. Picha: 26 May 2020Haki miliki ya pichaEPA
Image captionDonald Trump ameilaumu Twitter kwa kuingilia uchaguzi wa urais wa Marekani wa 2020
Bwana Trump amekuwa akiishutumu mitandao ya kijamii kila mara kuharihi sauti yake au hat ahata kuweka sauti ambayo hajazungumza lakini anakuwa anasikika kama yeye.
Jumatano, bwana Trump aliishutumu Twitter kwa kuingilia uchaguzi baada ya kuongeza maelezo ya tweet mbili kama uthibitisho.
Alhamisi , Twitter iliongeza taarifa za kuhakiki taarifa kuhusu Covid-19" na kujumuisha ujumbe wa tweet kutoka kwa msemaji wa serikali ya China anayedai kuwa virusi vya corona vilitengenezwa Marekani.

Amri hiyo inasemaje?

Amri hiyo imewekwa ili kufafanua sheria ya mawasiliano ya staha ambayo Marekani imeweka katika mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter na Youtube pamoja na ulinzi wa kisheria katika hali fulani.
Chini ya kifungu cha sheria cha namba 230, mitandao ya kijamii haiwajibishwi kwa maudhui ambayo watumiaji wake wanaweka mtandaoni lakini inaweza kuhusika kwa upande wa usamaria mwema wa kuondoa maudhui hayo mtandaoni ambayo labda yana maudhui ya unyanyasaji, chuki na yanahaibisha .
Amri hiyo maalumu inaainisha kuwa sheria ambayo italinda maudhui ya mitandao ya kijamii kama maudhui hayo hayajabilishwa kwa kuhaririwa na mtumiaji wa mtandao huo na kutaka sheria hiyo ibadilishwe au kuondolewa na wabunge kwa kifungu namba 230. Bwana Trump alisema mwanasheria mkuu William Barr ataanza mara moja kuandaa sheria ambayo itapigiwa kura.
Donald Trump's tweet and Twitter's warning sign below the postHaki miliki ya pichaTWITTER
Maamuzi hayo yanasema kuwa kuzuia maudhui ya mtu sio jambo la busara, pamoja na kujumuisha sababu ya kutochapisha maudhui hayo ambazo ziko tofauti na maelezo yaliyoandikwa katika sheria zilizopo kwenye huduma ya tovuti, amri hiyo mpya inataka lazima zilindwe.
Seneta wa Republican, Marco Rubio ni miongoni mwa watu wanaodai kuwa mitandao ya kijamii inachukua jukumu la mchapishaji hivyo wana haki ya kuongeza ukweli wa jambo katika baadhi ya machapisho.
"Sheria bado inalinda kampeni za mitandao ya kijamii kama Twitter kwa sababu wanajulikana kama jukwaa na sio wachapishaji," alisema bwana Rubio.
"Lakini kama wataamua sasa kufuata sheria za uhariri kama wachapishaji, basi watapaswa kutambuliwa kisheria kuwa wachapishaji."

Amri hiyo mpya inataka pia:

  • Kamati ya mawasiliano ya kitaifa (FCC) kutaja maudhui ambayo yamezuiwa kuchapishwa kwa madai ya watoa huduma kuwa wanalinda sheria na utaratibu ulioweka kwa kufungia maudhui ambayo si rafiki kwa umma.
  • Serikali kuangalia matangazo yake katika mitandao ya kijamii kurasa za mitandao ya kijamii na kuona kama yanakidhi marufuku yaliyopo.
  • White house kuanzishwa kwa teknolojia ambayo itaripoti ubaguzi ambao unafanyika katika mitandao ya kijamii.

Agizo hilo litakuwa na athari gani?

Donald Trump amehaidi kuchukua hatua kubwa dhidi ya maamuzi ya tweeter ya kuongeza ujumbe wa kuangalia ukweli wa jambo katika ujumbe wake.
Wakati tangazo la amri hiyo kutakiwa kuchukuliwa kwa uzito mkubwa na kuishutumu mitandao ya kijamii kwa kuwa na ubaguzi na kuhatarisha uhuru wa kuzungumza- itachukua muda mrefu kabla ya mazungumzo kuwa utekelezaji wa kweli, mkubwa au wa namna nyingine.
Wakala huru wa serikai watatakiwa kuangalia sheria zilizopo, kutangaza utaratibu mpya. Kuupigia kura na kuutetea mahakamani. Wakati wote huo, uchaguzi wa rais utakuja na kuondoka.
Hii inafafanua kwa nini rais Trump pia anahamasisha uwepo wa sheria mpya ambayo itapitishwa na watunga sheria na kuwa na namna ya moja kwa moja ya kubadili sera za Marekani katika kampuni za mitandao ya kijamii nchini Marekani.
Lengo kuu la amri ya rais, hata hivyo linaweza kuonekana kama ishara.
Kwa kiwango kidogo sana itafanya Twitter kufikiria mara mbili kuhusu kuangalia namna ya kujumuisha ukweli wa taarifa katika huduma zao.
Rais anategemea Twitter kuchapisha ujumbe wake bila kuongeza taarifa nyingine ambazo si zake.Kama Twitter itaanza kupunguza moja ya chombo chake cha mawasiliano, basi itakuwa inatuma ujumbe kuwa itajiondoa na kuweka vitu kuwa katika kiwango cha chini - na kampuni kutokuwa huru.

Mitandao ya kijamii imejibu vipi?

Twitter imeweka amri kuwa kujibu hatua hizo za kisiasa kwa kutumia taratibu za sheria pia, " aliongeza kuwa kifungu namba 230 "ambacho kinalinda uvumbuzi na uhuru wa kujieleza wa Marekani na kusisitiza umuhimu wa demokrasia".
Google, ambayo inamiliki YouTube, imesema kubadili kwa kifungu namba 230 kutaweza kuathiri uchumi wa Marekani na uongozi wa kimataifa katika uhuru wa mtandao.
"Tuna sera za wazi ya maudhui yetu na tunatekeleza bila kuangalia mitazamo ya kisiasa.
Majukwaa yetu yanasaidia idadi kubwa ya watu na kampuni mbalimbali ukiachilia mbali siasa, na kuwapa muongozo na namna mpya ya kuwasilisha kwa wafuatiliaji wao," aliiambia BBC.
Mkurugenzi wa Facebook bwana Mark Zuckerberg alihojiwa na Fox News, Jumatano na kusema kuwa katika suala la kuzuia maudhui yasichapishwe kwenye mitandao ya kijamii ni jambo ambalo serikali ilipaswa kuona kuwa jambo sahihi na kuhamasisha kufanyika badala ya kuwa na uhuru wa kujieleza.
"Nina Imani kubwa kuwa kama Facebook isingekuwa inahariri au kutoweka zuio la kila kitu ambacho wanaandika mtandaoni, hali ingekuwa mbaya," alisema bwana Zuckerberg.
"Nadhani kampuni binafsi zisingekuwepo labda katika majukwaa haya basi tusingekuwa katika nafasi ya kuendesha mitandao hii."
Wakati think tank ilionya kuwa amri hiyo inaweza kusababisha athari ambazo hazikutegemewa.
"Wakati huohuo, kampeni dhidi ya kampuni za mitandao ya kijamii ikiendelea basi wategemee athari kubwa kutokea katika uhuru wa kujieleza," alisema Matthew Feeney kutoka taasisi ya Cato.
Na kubadili sheria ya namna ya mawasiliano ya staha na kuweka utashi wa kisiasa katika kampuni za mitandao ya kijamii," unaweza kuona kuwa jukwaa hilo limeweka maudhui mengi ya kisheria ambayo kwa namna moja au nyingine wanataka kuondoa basi maudhui ya ngono , chuki na ubaguzi yatatawala bila kupingwa.
"Au wanaweza watachunguza maudhui kwa kiwango ambacho kinaweza kuathiri upatikanaji wa taarifa katika mitandao ya kijamii ambazo tumezoea kuzipata kwa sasa," alisema.
Bwana Feeney alisema mapendekezo ya amri hiyo ni upuuzi mtupu lakini ingeweza kuonyesha umaarufu wa kisiasa katika uchaguzi wa rais.

Post a Comment

0 Comments