Uchaguzi wa Burundi 2020: Vurugu na mauaji yakumba kampeini za uchaguzi Burundi

Mwanasiasa BurundiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Polisi nchini Burundi wamesema kuwa wamewakamata watu wapatao 64 kutoka chama kikuu cha siasa cha CNL, kumekuwa na ghasia pamoja na mauaji dhidi ya wanachama wa chama kikuu katika kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu wa rais tarehe 20 Mei.

Mgombea wa nafasi ya ubunge Cathy Kezimana, kutoka chama cha National Freedom Council (CNL) alikamatwa jana baada ya kufanya kampeni kusini mwa nchi hiyo.

Siku ya Jumanne, msemaji wa polisi Pierre Nkurikiye alikiambia chombo cha habari cha taifa kuwa vurugu nyingi na uhalifu katika kampeni unafanywa na wanachama wa CNL dhidi ya wapinzani wao CND-FDD, ambacho ni chama tawala.

Bwana Nkurikiye alisema ghasia hizo mpaka sasa zimesababisha wanachama wa chama tawala wawili kuuliwa na wengine 18 kujeruhiwa na mmoja hajulikani alipo na wanachama nane kutoka CNL wamejeruiwa.

"Uhalifu huu umefanywa zaidi na wanachama wa CNL wakiwa wanahamasishwa na viongozi wao .Kutokana na matukio hayo 64 kati yao wamekamatwa wakati uchunguzi ukiendelea." - alisema bwana Nkurikiye.

Msemaji wa CNL, bwana Terence Manirambona, aliiambia BBC kuwa wameshangazwa na maoni ya bwana Nkurikiye kwa sababu hawakutarajia kusikia maneno hayo kutoka kwake kwa kuwa wanategemea vyombo vya usalama kuwa na haki sawa kwa wote".

Bwana Manirambona alisema wanachama wa chama chake wamekuwa wahanga wa vurugu hizo na unyanyasaji ulioanza hata kabla ya kampeni kuanza.

Uchaguzi kufanyika katika kipindi cha wiki mbili licha ya hofu ya janga la coronaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUchaguzi kufanyika katika kipindi cha wiki mbili licha ya hofu ya janga la corona

"Tangu kampeni zianze, wanachama wetu wengi walikamatwa kwa madai ambayo hayana ukeli, wawili walipotea na wengi walijeruhiwa katika ghasia hizo ambazo zimeanzishwa na wanachama wa chama tawala ambao waliingilia shughuli zetu," - bwana Manirambona aliiambia BBC.

Bwana Manirambona alisema bi.Cathy Kezimana alikamatwa jana lakini polisi hawajamwambia sababu ya kukamatwa kwake mpaka leo hii.

"Tumesikia tu amepelekwa gerezani , yeye ni miongoni mwa wengi ambao wamekamatwa bila hatia " - bwana Manirambona alisema.

Chama tawala na wapinzani wao CNL ndio wagombea wakuu wa uchaguzi mkuu wa Mei, 20, wagombea saba wanawania nafasi ya uraisi na wengine ubunge na manispaa.

Jumatatu katika mji wa Gitega watu walikua wemejaa kiasi cha kubaba wakati wa kampeni za mgombea wa chama tawalaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJumatatu katika mji wa Gitega watu walikua wemejaa kiasi cha kubanana wakati wa kampeni za mgombea wa chama tawala

Post a Comment

0 Comments