Umoja wa Mataifa waomba dola bilioni 4.7 kupambana na janga la COVID-19

Umoja wa Mataifa umetoa ombi jipya la dola bilioni 4.7 kwa ajili ya kuwalinda mamilioni ya watu na kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya korona katika mataifa yaliyo na hali mbaya zaidi duniani.

 Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya kibinaadamu, Mark Lowcock, amesema kwamba machungu makubwa zaidi ya janga la COVID-19 yatakuwa mataifa yaliyo masikini zaidi duniani, na kwamba bila ya kuchukuwa hatua madhubuti hivi sasa, dunia inapaswa kujitayarisha kwa ongezeko la migogoro, njaa na umasikini.

Fedha hizo ni kando ya zile dola bilioni 2 ambazo tayari Umoja wa Mataifa ulikuwa umeziomba wakati ulipozinduwa mpango wake wa huduma za kibinaadamu tarehe 25 Machi.

Hadi sasa, umeweza tu kukusanya nusu ya kiwango hicho. Idadi kamili ya dola hizo bilioni 6.7 kinatazamiwa kugharamia mpango wa huduma za kibinaadamu kutoka sasa hadi mwezi Disemba.

Post a Comment

0 Comments