tangazo

Usafiri wa treni kati ya Ujerumani na Paris kuanza tena

Huduma ya treni kati ya miji mikuu ya Ufaransa na Ujerumani itaanza tena leo, kampuni ya taifa ya reli nchini Ujerumani imetangaza.

 Safari ya masafa marefu kutoka Frankfurt hadi Paris kupitia Saarbrueken itaanza tena kwa kutumia treni iendayo kasi ya ICE kutoka pande zote kila siku, msemaji wa Shirika la reli la Ujerumani Deutsche Bahn amesema.

Usafiri kwenda Ufaransa, ambayo imelegeza hatua za kuwazuwia watu kutoka majumbani mwao kuanzia leo Jumatatu, inaruhusiwa tu kwa watu wenye sababu muhimu kuvuka mpaka, kama kwenda kazini ama shule.


ADVERTISEMENT

Post a Comment

0 Comments