tangazo

Uturuki yakanusha tuhuma za kutishia usalama helkopta aliyokuwemo Waziri wa ulinzi wa Ugiriki

Uturuki imekanusha tuhuma ambazo zimetolewa na waziri wa ulinzi wa Ugiriki Nikos Panagitopoulos.

Waziri wa ulinzi wa Ugiriki amelituhumu jeshi la Uturuki  kutishia usalama helikopta aliokuwemo .

Waziri huyo wa Ulinzi wa Ugiriki ametuhumu jeshi la anga la Uturuki kumtishia usalama kwa kutumia ndege zake za kivita.

Msemaji wa  wizara ya mambo ya nje ya Uturuki Hami Aksoy  ametoa taarifa  kuhusu  tuhuma hizo zilizotolewa na waziri wa ulinzi wa Ugiriki  kwa kufahamisha  kwamba jeshi la Uturuki lilikuwa katika kuetekeleza wajibu wake wa kila siku katika bahari ya Egean.

Hami Aksoy katika ujumbe wake  huo ambao amekanusha tuhuma  kutoka kwa waziri wa Ulinzi wa Ugiriki amesema kwamba haina nama kwa Uturuki kumtishia amani waziri wa Ulinzi wa taifa mshirika , ni wajibu wa Ugiriki kuwa na imani na washirika wake  wakati wakiendesha shuhuli zao za kila siku kulinda mipaka.

Post a Comment

0 Comments