Uturuki yatuma msaada wa pili wa vifaa vya matibabu Marekani

Uturuki imetuma msaada wake wa pili wa vifaa vya matibabu nchini Marekani katika juhudi za kupambana na virusi vya corona.

Uturuki imefahamisha kutuma msaada wa vifaa vya matibabu na madawa nchini Marekani katika jitihada za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona.

Marekani ndio taifa la  kwanza ulimwenguni lililoathirika kwa kiasi kikubwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Msaada huo kutoka Uturuki kuelekea nchini Marekani ni msaada wa pili baada ya kutuma msaada wa kwanza ulopokolewa nchini humo na kutoa shukrani kwa Uturuki kwa kuonesha ushirikiano wake akatika kipindi hiki kigumu.

Msaada huo ni pamoja na  barakoa, barakao maalumu aina ya N95,  mavazi maalumu kwa wauguzi ya kujikinga na maambukizi, vimiminiko  vya kuanagamiza vimelea nba kuzuia maambukizi ya covid-19.

Ndege hiyo kutoka Uturuki imeripotiwa kuwasili katika uwanja wa ndege wa  Andrews nchini  Marekani.

Msaada huo umetolewa nchini Marekani katika juhudi za kupambana na maambukizi ya virusi vya corona na  kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya mataifa hayo mawili.

Ndege hiyo imepakia mzigo huo  katika uwanja wa ndege wa   jeshi wa EtÄŸmesgut mjini Ankara  akihudhuria  makamu waziri wa mambo ya nje wa  Uturuki Yavuz Selim Kıran na balozi wa Marekani mjini Ankara David Satterfield.

Post a Comment

0 Comments