tangazo

UWT Mkoa wa Ruvuma yatoa vifaa kupambana na corona

Umoja wa wanawake chama cha mapinduzi mkoa wa Ruvuma bi.Kuluthumu Mhagama ambae ni mwenyekiti wa UWT wametoa msaada wa vifaa vya kupambana na ugonjwa wa covd19 kwa mkuu wa mkoa  Ruvuma bi.Christina  Mndeme.

Bi.Kuluthumu amesema kama mwenyekiti wa UWT mkoa wanaungana na serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona kwa kutoa ndoo za maji, sabuni pamoja na vitakasa mikono ambavyo vimegharimu kiasi cha shilingi laki tano.

Akipokea vifaa hivyo mkuu wa mkoa bi.Christina Mndeme amewashukuru jumuiya ya wanawake chama cha mapinduzi mkoa kwa kujitoa kwao kuunga mkono Juhudi za serikali kupambana na ugonjwa wa covd19 amesema vifaa walivyo toa vitaenda kufanya kazi iliyo kusudiwa pia bi.Mndeme amewakabidhi jeshi la magereza vifaa hivyo ili vikawasaidie nao kujilinda dhidi ya corona.

Akishukuru kwa niaba ya jeshi la mageraza kamishna msaidizi Alexander Nyefwe amesema vifaa hivyo vita wasaidia wafungwa na askari pia na atavisambaza katika mageraza yote yaliyopo mkoa Ruvuma kwa uwiano sawa kwa kila gereza.

Post a Comment

0 Comments