tangazo

Vifo vya corona Marekani vyazidi elfu 76

Hadi mapema leo hii vifo vitokanavyo na Virusi vya corona Nchini Marekani vimefikia 76,938 na visa 1,292,623 ikiwa ndiyo Nchi inayoongoza Duniani kwa wagonjwa na vifo.

Hispania visa 256,855 na vifo 26,070, Italia visa 215,858 na vifo 29,958, Uingereza visa 206,715 na vifo 30,615 ikiwa ndiyo Nchi inayoongoza kwa vifo vya corona kwa Bara la Ulaya.

Kwa Nchi za Afrika, Afrika Kusini bado inaongoza kwa visa vingi vya corona ikithibitisha wagonjwa 8,232 na vifo 161, Egypt visa 7,981 na vifo 482, Morocco visa 5,548 na vifo 183 na Algeria visa 5,182 na ikiongoza kwa vifo kwa upande wa Afrika ikiwa na vifo 483.

WHO imesema kati ya watu 83,000 hadi 190,000 Barani Afrika wanaweza kufariki kwa corona na huenda pia watu milioni 29 hadi milioni 44 wakapata maambukizi ya virusi vya corona ndani ya mwaka mmoja wa kwanza wa janga hili iwapo kama virusi hivyo havitodhibitiwa

Post a Comment

0 Comments