Vifo vya COVID-19 vyapindukia 300,000 Duniani kote

Idadi ya vifo vilivyotokana na maambukizi ya virusi vya corona duniani kote imepindukia watu 300,000, ambapo vingi vya vifo hivyo vimetokea Ulaya na Marekani, tangu kuzuka kwake huko China, mwishoni mwa mwaka uliopita.
Marekani ndio yenye visa vingi kwa kuwa na vifo 85,194, ikifuatiwa na Uingereza vifo 33,614, Italia vifo 31,368, Ufaransa vifo 27,425 na Uhispania yenye vifo 27,321.
Brazil imesajiri maambukizi mapya ya virusi vya corona 13,944 na vifo 844. Rekodi hizo zimetolewa na wizara ya afya zinawakilisha katika kipindi cha masaa 24. Idadi jumla tangu kuanza kwa mripuko huo ni maambukizi 202,918 na vifo 13,933. Katika eneo hilo hilo la Amerika ya Kusini Imerekodi vifo vipya 257 na maambukizi 2,409. Kiwango hicho kikitajwa kuwa cha juu zaidi tangu kuingia kwa maambukizi hayo nchini humo. Taarifa hizo mpya zinafanya jumla ya maambukizi kufikia 42,595 na vifo 4,477.

Rais wa Macron kukutana na mkuu wa kampini ya utafiti wa chanjo

 Emmanuel Macron wa Ufaransa

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa Mei 19 atakutana na Mtendaji Mkuu wa kampuni kubwa ya kutengeneza madawa-Sanofi, Paul Hudson, baada ya siku chache zilizopita mkuu huyo kuigadhibisha serikali, kwa kusema baadhi ya mataifa yatapewa kupaumbele katika upatikanaji wa chanjo ya virusi vya corona. Hudson aliifuta kauli yake hiyo ya awali, mapema Alhamis kwa kusema ni muhimu kwamba chanjo yoyote ya corona, ikifika kwa wote katika pembe tofauti za ulimwengu.
Mkuu wa Shirika la Afya Duniani kwa Ulaya, Hans Kluge amesema kasi ya usambaaji wa virusi vya corona kwa Ulaya, inapungua, lakini ameongeza kuwa lazima mataifa yaendelea kuwa madhubuti katika kukabiliana na janga hilo. Amesema funzo lililopo kwa sasa ni kwamba hakuna muda wa kusherehekea, lakini muda wa kujiandaa.

Post a Comment

0 Comments