Virusi vya corona: Hospitali za Uingereza zaanza kufanyia majaribio dawa mpya

Kaye Flitney mmoja wa watu 75 waliorodheshwa kufanyiwa majaribio ya chanjo
Kaye Flitney ni mmoja wa watu waliojitolea kujumuishwa katika majaribio ya dawa mpya ya kukabiliana na virusi vya corona.
Dawa mpya iliotengenezwa na wanasayansi wa Uingereza kutibu Covid 19 inafanyiwa majaribio katika chuo kikuu cha Southampton.
Ikiwa imetenegenezwa na kampuni ya Synairgen , inatumia protini kwa jina infterferon beta, ambayo hutoka katika mwili wa binadamu anapopata maambukizi ya virusi.
Matokeo ya majaribio hayo yanatarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwezi Juni.
Kwa sasa kuna dawa chache zinazoweza kutibu virusi hivyo huku madaktari wakitegemea kinga ya wagonjwa wao.

Je ni dawa gani hiyo?

Interferon beta ni dawa inayolinda mwili wa binadamu dhidi ya virusi, ikionya dhidi ya shambulio la virusi , kulingana na Richard Marsden , afisa mkuu mtandaji wa kampuni ya Synairgen iliopo na makao yake mjini Southampton.
Anasema kwamba virusi vya corona hujaribu kukabiliana na uzalishaji wake kama mpango wa kutaka kukwepa mfumo wa kinga mwilini.
Dawa hiyo ina muundo maalum wa interferon beta inayowekwa moja kwa moja kwenye njia za hewa wakati zilizopo na virusi, kwa matumaini kwamba kipimo cha protini moja kwa moja kitatoa majibu ya kupambana na virusi hata miongoni mwa wagonjwa ambao kinga zao tayari ni dhaifu.
Interferon beta hutumika sana kutibu ugonjwa wa kupooza. Synairgen tayari imethibitisha kwamba maandalizi yake yanaweza kuimarisha kinga katika mapafu ya mgonjwa mwenye asthma na magonjwa sugu ya mapafu.
Lakini tunaweza kujua iwapo inaweza kukabiliana na Covid-19 baada ya kufanyiwa majaribio kadhaa miongoni mwa binadamu.

Mgonjwa

Kaye Flitney ni miongoni mwa wagonjwa waliojumuishwa katika majaribio hayo yaliorekodiwa na BBC panorama .
Inahitaji wagonjwa wa Covid-19 kama yeye, kuvuta dawa hiyo kwa kutumia nebulizer ili kuuingiza katika mapafu.
Kaye, 67, anapata shida kuketi katika kitanda chake cha hospitali na anakohoa anapoweka dispenser katika mdomo wake.
Anasema kwamba mara ya kwanza alipogundua ana virusi vya corona mafikra yake ya kwanza yalikuwa sio kuangalia afya yake.
''Nilitishika kwasababu mume wangu ana tatizo la moyo. Itamuua''.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 67, ambaye alipelekwa hospitalini kutokana na tatizo la kupumua , alisema kwamba utumizi wa dawa hiyo haujamsababishia tatizo lolote.
''Huwezi kujua kwamba unaitumia hadi pale utakapomaliza. Sio mbaya. Naweza kuitumia nyumbani''. Je vipimo hivyo vinafanyika vipi?
Watu 75 waliojitolea kufikia sasa walitoka katika hospitali 10 nchini Uingereza .
Nusu yao watapatiwa dawa hiyo huku wengine waliosalia wakipatiwa dawa kama hiyo lakini ya bandia.
Hakuna anayehusishwa katika majaribio hayo anajua ni wagonjwa gani waliopatiwa dawa ya aina gani hadi pale vipimo hivyo vitakapokamilika.
''Iwapo utajua kwamba ni dawa unaweza kuwa na upendeleo'', anaelezea sandy Aitken, muuguzi anayetoa dawa hiyo.
Matumaini ni kwamba , itaonyesha kwamba wagonjwa wanaopatiwa dawa hiyo wanaimarika ikilinganishwa na wale ambao hawakupatiwa, kulingana na Profesa Tom Wilkinson , wa chuo kikuu cha Southampton.
Justin Rowlatt na Sandy AitkenHaki miliki ya pichaBBC PANORAMA
Image captionMwandishi wa BBC Justin Rowlatt na muuguzi Sandy Aitken wakiwa kando ya kitana cha mgonjwa
Majaribio ya dawa ya kampuni ya Synairgen ni mojawapo ya vipimo vya haraka vilivyoanzishwa na serikali.
Mpango huo kwa jina Accord kama unavyojulikana unalenga kutengeneza dawa mpya ya wagonjwa wa corona.
Awamu ya kwanza itashirikisha dawa nyengine sita.
Zaidi ya tiba 100 kote duniani zinafanyiwa majaribio na dawa kwa jina remdesivir ambayo ilitengenezwa kutibu ebola imeonyesha matumaini.
Maafisa wa Marekani wamedai kwamba kuna ushahidi wa moja kwa moja kwamba inaweza kuwaponya watu walio na virusi vya corona.

Je tiba hiyo itakamilika lini?

Matokeo ya awali ya interferon beta yanatarajiwa mwisho wa mwezi Juni.
lakini hata iwapo dawa hiyo itaonyesha matumaini, itafanyiwa uchunguzi zaidi kabla ya kuanza kutumika miongoni mwa wagonjwa.
Hatua hiyo huenda ikachukua miezi kadhaa, ijapokuwa serikali itafanya kazi haraka iwezekanavyo.
Iwapo itaonekana inafanyakazi, dawa hiyo pamoja na kifaa kinachotumika kuivuta mapafuni italazimika kutengenezwa kwa wingi.
Bwana Marseden anasema kwamba tayari anazungumza na wasambazaji kote duniani iwapo itawezekana kuanza kuzalisha dawa hiyo punde tu majaribio hayo yatapokamilika.
Hatahivyo , anasema kwamba haitaweza kupatikana hadi mwisho wa mwaka.
Pia unaweza kutazama Panorama: Tutakuwa Salama Lini? saa19:30 BST Jumatatu, katika BBC One na BBC iPlayer.

Post a Comment

0 Comments