Virusi vya corona: Itakua ni ''uendawazimu'' kuendesha uchaguzi wakati wa corona, asema rais wa Uganda

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kuwa itakua ni 'uendawazimu' kuendesha uchaguzi wakati wa mlipuko wa virusi vya corona.

Ameliambia shirika la habari la Uganda NBS kwamba mipango ya kufanya uchaguzi mapema mwaka 2021 haitakuepo kama virusi vya corona havitadhibitiwa itatakiwa kuangaliwa upya.

Kuna jumla ya visa 122 vya Covid-19 vilivyothibitishwa nchini Uganda.

Mikutano ya umma mkiwemo ya kisiasa imepigwa marufuku kama sehemu ya hatua za kutosogeleana na kukaa nyumbani zilizowekwa nchini humo kwa ajili ya kuzuwia kusambaa kwa virusi vya corona.

Takriban wagombea 24 wametangaza nia yao ya kugombea kiti cha urais na wamewasilisha maombi yao kwa Tume ya Uchaguzi ili kukabiliana na rais Museveni na wameanza mikutano ya kitaifa.

Mikutano hii imeahirishwa kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.


ADVERTISEMENT

Kauli za Bwana Museveni sasa zimeibua swali juu ya ikiwa mchakato mzima wa uchaguzi utaahirishwa au la.

Mwanamuziki na Mbunge Bobi Wine

Uchaguzi wa mwaka ujao unatarajiwa kuwa wa mchuano mkubwa hususan kati ya mgombea mwenye umri wa miaka 38 Mwanamuziki na Mbunge Bobi Wine ambaye ameonekana kuwa mpinzani mkuu dhidi ya Bwana Museveni ambaye amekua mamlakani tangu mwaka 1986.

Kumekua na maswali juu ya ni kwa kiwango gani uchaguzi huo utakua ni wa haki na huru huku kukiwa na shutuma kwamba wapinzani wa Museveni walikabiliwa na vitisho.

Jenerali mstaafu , Henry Tumukunde, ambaye alitangaza mipango ya kukabiliana na Museveni ambaye alikua mshirika wake zamani pia ameshitakiwa kwa mashtaka ya uhaini na kuachiliwa kwa dhamana siku ya Jumatatu baada ya kukaa jela miezi miwili.

Virusi vya corona: Wakenya wabuni mbinu tofauti ya kufanya ibada nyumbani

Post a Comment

0 Comments