tangazo

Virusi vya corona: Je kuwa mnene kupindukia kunaweza kuongeza hatari?

Kuwa mnene wa mwili wa kupindukia kunafahamika kuongeza hatari ya mtu kupata magonjwa kadhaa, mkiwemo magonjwa ya moyo na kisukari aina ya pili.

Utafiti wa awali unasema huenda unene wa kupindukia ukawafanya walio na Covid-19 kuugua zaidi , lakini ni kwanini iwe hivyo?

Je kuna ushahidi kwamba unene wa kupindukia ni hatari unapokua na virusi?

Swali hili limefanyiwa utafiti na tafiti nyingi huku watafiti na wataalamu wakijaribu kufanya tafiti nyingi wakijaribu kufanyia kazi jibu.

  • Katika utafiti wa hospitali 17,000 zenye wagonjwa wa corona nchini Uingereza, wale wenye unene wa kupindukia wenye ukubwa wa mwili kwa kiwango cha (BMI) ya zaidi ya 30 - walikua na uwezekano wa 33% wa kufa kuliko wale wasio na unene wa mwili wa kupindukia.
  • Utafiti tofauti wa hutuma za afya za taifa nchini Uingereza ilibainika kuwa kuna hatari mara dufu za kufa kutokana na Covid-19 miongoni mwa watu wenye unene wa mwili wa kupindukia. Kama matatizo mengine ya kiafya yalihusika na unene wa kupindukia mfano ugonjwa wa moyo na kisukari aina ya 2 vilizingatiwa na ilibainika kuwa hatari iliongezeka na kuwa ya kiwango cha juu zaidi , watafiti walisema.
  • Na utafiti uliofanyika kwa wagonjwa mahututi nchini katika vitengo maalum vya wagonjwa mahututi ulibaini kuwa karibu 34.5% walikuwa wanene, 31.5% walikua wanene kupindukia na 7% walikua sio wanene (jumla 73%), ikilinganishwa na 26% waliokua na kipimo kinachofaa kiafya cha unene -BMI.

Unaweza pia kutazama:

Virusi vya corona:Vidokezo tano ya jinsi ya kuimarisha afya yako ya kiakili

Kutokana na viwango vya juu vya watu wenye unene wa kupindukia wa mwili duniani, shirikisho la watu wenye unene wa kupindukia dunaini -World Obesity Federation, linasema asilimia kubwa ya watu waliotaka usaidizi kuhusu virusi vya corona walikua ni wenye unene wa kupindukia "walikua pia na BMI zaidi ya 25". Tafiti za awali kutoka Marekani, Italia na Uchina pia zilionyesha kuwa unene wa kupindukia ni sababu ya hatari.

Utu uzima, kwa mwanaume na mwenye matatizo ya kudumu ya afya vyote huongeza hatari za kuugua sana kutokana na Covid -19.  

Ni kwanini unene wa mwili wa kupindukia ni hatari?

Kadri unavyokua na uzito wa kupindukia wa mwili ndivyo unavyokua umebeba kiwango kikubwa cha mafuta mwilini, kadri unavyokosa kufanya mazoezi ya mwili, ndivyo uwezo wako wa mapafu unavyopungua . Hii inamaanisha kuwa mwili wako unahangaika kuingiza hewa safi ya oksijeni ndani ya damu na sehemu nyingine za mwili mzima. Hii inaathiri moyo na mzunguko wa damu mwilini.

Kwasababu watu wanauzito wa mwili wa kupindukia, pia wanahitaji oksijeni k mwilini . Kwahiyo hii inamaana miili yao inapitia shinikizo kubwa ," anasema Profesa Naveed Sattar, Kutoka Chuo Kikuu cha Glasgow. Wakati wa maambukizi kama virusi vya corona inawesza kuwa hatari.

Fat cells in adipose tissueHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Seli za mafuta zina mchango gani?

Wanasayansi waligundua kuwa kimeng'enyo kinachojulikana kama ACE2, ni njia kuu ya virusi ya kuingia mwilini. p

Kiasi kikubwa cha kimeng'enyo hiki hudhaniwa kupatikana katika nyama za mafuta, ambazo watu wenye unene wa kupindukia huwa wanacho -chini ya ngozi na kuzingira viungo vyao vya mwili.

Hiyo inaweza kuwa mojawapo ya sababu wana hatari kubwa ya kuugua sana kutokana na mafuta hayo

Uwezo wa mwili wa kupambana na virusi- unaofahamika kama jibu la kinga-sio mzuri kwa watu wanene kupindukiaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUwezo wa mwili wa kupambana na virusi- unaofahamika kama jibu la kinga-sio mzuri kwa watu wanene kupindukia

Je mfumo wa kinga unaathiriwa pia ?

Zaidi ya yote, uwezo wa mwili wa kupambana na virusi- unaofahamika kama jibu la kinga-sio mzuri kwa watu wanene kupindukia.

Hii hutokana na kuumia kunakosababishwa na seli zinazojulikana kama macrophages kwa lugha ya kitaalamu ambazo huvamia nyamanyama za mafuta mwilini. Huingilia mfumo wetu wa seli za kupambana na virusi .

Kwa mujibu wa wanasayansi, hii inaweza kusababisha matatizo makubwa ya kuugua yanayotokana na kuumia kunakotokana na virusi na madhara makubwa.

Aina ya kipekee ya nyama ya mafuta hutokana na uvamizi huo wa macrophage . Hii ndio maana watu weusi, Waafrika na watu kutoka jamii za walio wachache, wenye aina hizi za nyama za mafuta , "wamekua wakipata zaidi viwango vikubwa vya ugonjwa wa kisukari s," anasema Dkt Sellayah

London ambulanceHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Je kunaweza kuwa na matatizo mengine yaliyojificha?

Mara nyingi unene wa kupindukia huja na matatizo mengine ya kiafya s kama vile magonjwa ya moya na mapafu, figo na kisukari yaina ya 2 r

Kuganda kwa damu kunaweza pia kutokea, lakini haijajulikana ni kwani.

Post a Comment

0 Comments