Virusi vya Corona: Je, nchi za Afrika zimeweza kuzuia kasi ya maambukizi?

Rais Yoweri Museveni ametangaza kuwa kuvaa barakoa ni jambo la lazima nchini humo kuanzia leo katika kipindi hiki ambacho marufuku ya kutotoka nje inalegezwa.
Hatua hiyo ilitangazwa Jumatatu usiku ambapo rais Museveni alihutubia taifa baada ya kumaliza siku 35 za marufuku ya kutotoka nje ama 'lockdown'.
Museveni amesema watu wanaweza kuvalia mpaka barakoa ambazo zimeshonwa kienyeji na vitambaa.
Hata hivyo, kumekuwa na mashaka kutoka kwa wataalamu wa afya juu ya ufnisi wa barakoa za kutengenezwa nyumbani.
Katika hatua nyengine, Museveni amesema kuwa kuruhusu shughuli kuendelea kama awali inabidi kufanyike kwa umakini na mpangilio ili kuzuia virusi kusambaa kwa kasi.
Kwa kuanzia, ameruhusu maduka ya jumla, karakana za kukarabati magari, maghala kufunguliwa. Pia ameruhusu wafanyakazi wa bima na idadi ndogo ya wanasheria kurejea kazini.
Masharti mengine yaliyosalia ya marufuku ya awali bado yanaendelea mathalani kufungwa kwa mipaka ya nchi, kutoruhusu usafiri binafsi na wa umma, mikusanyiko ya watu na marufuku ya kutotoka nje usiku bado yangalipo kwa kipindi kingine cha siku 14.
Museveni amesema hatua hizo mpaka sasa zimetoa mafanikio ambayo ni kuzuia kusambaa kwa kasi kwa virusi hivyo.
"Hauwezi kuacha kulala kwa kuota ndoto mbaya. Tutaanza kufunguka taratibu bila ya kuharibu mafanikio yetu. Mafanikio hayo ni wagonjwa 89, waliopona 55 na hakuna kifo hata kimoja," ameeleza Museveni jana usiku.
Idadi mpya ya maambukizi kufikia leo asubuhi nchini humo imeongezeka kutoka 89 mpaka 97.
Kati ya wagonjwa hao, Waganda ni 57. Mpaka kufikia Jumatatu, madereva 30 wa malori walikuwa wamekutwa na corona nchini humo, kati yao Wakenya 13 na Watanzania 12.
Hatua ya Uganda kulegeza masharti ya marufuku hizo yanaendana na Rwanda na Nigeria ambazo kuanzia jana asubuhi zilifanya hivyo. .
Maisha yarejea katika hali ya kawaida Rwanda
Mabasi kubeba idadi nusu ya idadi ya awali
Image captionMabasi kubeba idadi nusu ya idadi ya awali Rwanda
Baada ya siku 45 za kusalia ndani mjini kigali, kulikuwa na shughuli nyingi hapo jana, Raia wa Rwanda walirejelelea shughuli zao kwa masharti ya kuvaa barakoa na kutokaribiana.
Serikali imelegeza masharti iliyochukua kwa misingi ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.
Serikali ya Rwanda ilitangaza kwamba kuanzia Jumatatu 04/05/2020, baadhi ya watu wataruhusiwa kuendeleza shughuli zao za kawaida, huku baadhi zikiendelea kufungwa.
Taarifa ilisema kuanzia Jumatatu wakaazi wataruhusiwa kufanya kai zao lakini hawataruhusiwa kuondoka majumbani kuanzia saa mbili usiku hadi kumi na moja asubuhi.
Biashara za umma na kibinafsi pia zitafunguliwa tena, masoko yatafunguliwa tena lakini ni asilimia 50 pekee ya wafanyabiashara ndio watakaofanyakazi.
Migahawa na hoteli zitaanza kufanyakazi na kufungwa kuanzia saa moja usiku.
Aidha, wanariadha wataruhusiwa kufanya mazoezi lakini michezo mengine mikubwa na majumba mengine ya burudani yataendelea kufungwa.
Kulingana na mwandishi wa BBC raia walikuwa wengi sana katika mji wa Kigali.
Katika mji wa Kigali, watu walionesha kufurahishwa na hatua ya kurejea katika maisha ya kawaida lakini kupanda kwa nauli ni jambo ambalo limekera wengi.
Serikali imeongeza nauli kwasababu mabasi yanaruhusiwa tu kubeba idadi nusuya watu kama hatua moja ya kuhakikisha kutokaribiana kunatimizwa, serikali imesema.
Rwanda
Image captionWatu wakisubiri usafiri katika mji wa Kigali
Je, Rwanda wanatekeleza vipi hatua ya kuondosha marufuku?
Mikusanyiko bado imepigwa marufuku na kila biashara inayofanywa inatakiwa kutozidisha nusu ya wanaofanya biashara hiyo. Sheria ya kutotoka nyumbani imelegezwa kutokana na kile kinachoonekana kuwa shinikizo za kiuchumi baada ya kutekelezwa kwa zaidi ya wiki sita.
Mwandishi wa BBC Yves Bucyana anaripoti kutoka Kigali kuwa Rwanda kuwa biashara nyingi zikiwemo hoteli na migahawa zimefungua tena milango.
Hata hivyo kuna mpango maalumu wa kuhakikisha kuwa licha ya biashara hizo kufunguliwa lakini hazihatarishi kusambaa kwa virusi.
Miongoni mwa biashara zinazorejea leo hizo ni usafiri wa umma ambapo kwa sasa mabasi yanatakiwa kubeba nusu ya idadi ya abiria tu na si vinginevyo.
Magari hayo tayari yameshawekwa alama wapi mtu akae na wapi mtu asikae.
Katika vituo vya mabasi abiria waliovalia barakoa wameonekana wakipanga foleni kwa kuweka mwanya wa mita moja baina yao kama hatua mojawapo ya kujilinda.
Kulingana na waziri wa biashara na viwanda wa Rwanda Bi Soraya Hakuziyaremye wafanyabiasha hasa kwenye masoko na wengine wanaofanyabiashara kwa mkusanyiko watalazimika kufanya kazi kwa kupokezana ili kutimiza masharti ya kujilinda na virusi vya corona.
"Tunalazimisha kila soko kuwa na asilimia 50 tu ya wachuuzi,wanaweza kufanyabiashara kwa zamu baadhi wakifanya kazi leo wengine kesho.tutahakikisha kila jengo la biashara linafanya kazi kwa kufwata utaratibu huo .Tumefungua kidogo tu lakini pia hatutaki kupata mlipuko mpya wa virusi kwa sababu ya kuachilia biashara"
Shughuli zote zitatakiwa kufunga angalau saa moja kabla ya kuanza kwa sheria ya kutotoka nyumbani inayoanza kutekelezwa saa mbili za usiku hadi kumi na moja alfajiri.
Hata hivyo vilabu vya pombe, shule, usafiri wa boda boda na mikusanyiko ya watu ikiwemo makanisa pamoja na safari za mkoa hadi mwingine bado ni marufuku.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na BBC wamekaribisha hatua ya kulegeza masharti ya kutotoka nyumbani.
"Ni furaha kubwa kutoka nje,kuna mambo mengi ambayo yalikuwa yanaharibika hasa biashara.lakini sasa hivi mtu amepata afueni ya kutoka nje,mtu sasa anaweza kupumua,'' ameeleza Kigenza Rogers
Kuhusu hali ya maambukizi ,takwimu za hadi kupikia leo zinabainisha kwamba idadi ya wagonjwa waliopo katika vituo vya matibabu ya Covid 19 ni 135 ilhali waliopona ni 124, hakuna aliyefariki.
Nigeria kuanza na shughuli za kiuchumi
Nigeria kuanzia Jumatatu itaanza kulegeza masharti ya kusalia ndani katika mji mkuu wa Abuja, na mji mkubwa kabisa wa Lagos, katika jaribio la kupunguza athari ya kiuchumi barani Afrika.
Nigeria imeongeza idadi ya waopimwa kwa siku kote nchini humo
Image captionNigeria imeongeza idadi ya waopimwa kwa siku kote nchini humo
Serikali imesema kurejelelea shughuli za kiuchumi ni awamu ya kwanza ya mchakato utakaochukua wiki sita. Imeongeza kuwa hali hiyo itatathminiwa tena katika kipindi cha wiki mbili zijazo na iwapo hali itakuwa shwari, hatua ya kusalia ndani itaondolewa kabisa.
Maduka na masoko kwasasa yatafunguliwa hadi mchana na inatarajia kwamba baadhi ya watu wataweza kurejea kazini.
Lakini marufuku ya mikusanyiko ya watu bado inaendelea na pia hatua ya kutotoka nje kuanzia saa mbili usiku hadi kumi na mbili asubuhi itaendelea.
Shule na maeneo ya kuabudu bado yamefungwa.
Kuvaa barakoa unapokuwa kwenye maeneo ya umma na watu kufuata kanuni ya kutokaribiana na hatua za zote za kiusalama ni lazima.
Usafiri baina ya maeneo pia kumeahirishwa isipokuwa tu kwa wafanyakazi ambao ni lazima.
Nchi hiyo imekuwa na ongezeko kubwa la watu wanaoathirika na virusi vya corona katika kipindi cha wiki moja iliyopita huku idadi jumla ya walioathirika ikifikia 2,558 na vifo 87.
Mji wa Lagos kusini magharibi bado ni kitovu cha janga la corona, idadi jumla ya walioathirika ikifikia 1,068.
Mji wa Kano kaskazini mwa Nigeria umeekodi waathirika 313 huku Abuja ikithibitisha waathirika 266.
Elise Mukamabano alipanda basi kuelekea mji wa Kigali, umbali wa kilomita 20 anakofanyakazi katika mgahawa mmoja, ila nauli ya safari yake moja kwa sasa ni mara mbili ya kile alichokuwa akilipa awali.
"Huu n mzigo mwengine baada ya watu kusalia nyumbani kwa zaidi ya mwezi mmoja"- ameiambia BBC.
Hadi kufikia sasa, Rwanda imerekodi watu 259 walipata ugonjwa wa Covid-19 huku wengine 124 wakipona na hakuna hata mmoja aliyekufa kwasababu ya virusi vya corona.
Banner
Nchini Kenya migahawa ya imefunguliwa
Wahudumu watahitajika kuvaa barakoa, kutumia vitakasa mikono na kutokaribiana umbali wa mita 1.5
Image captionWahudumu watahitajika kuvaa barakoa, kutumia vitakasa mikono na kutokaribiana umbali wa mita 1.5
Waziri wa Afya nchini Kenya Mutahi Kagwe alitangaza masharti mapya ya uendeshaji migahawa kama njiamoja ya kulegeza masharti ili kufufua uchumi.
Migahawa kuanza kufunguliwa kuanzia saa 11 asubuhi na 10 jioni.
Watakaoingia kuhudumiwa watahitajika kufuata utaratibu uliopo wa kunawa mikono, kutumia vitakasa mikono na kuvaa barakoa kama kawaida. Hatua ya kutokaribiana itaendelea kutekelezwa umbali wa mita 1 baina ya mtu mmoja hadi mwengine.
Lakini watakaoruhusiwa kutoa huduma ni wale watakaokuwa wamepimwa pekee.
Pia kulingana na wizara ya afya, katika migahawa hiyo, huduma ya kujiwekea chakula bado imesitishwa.
Wizara hiyo imetoa agizo la watu wote wanaoingia migahawani kupimwa kiwango cha joto na kuruhusiwa tu kuingia ikiwa litakuwa chini ya nyuzi 37.5 na mgahawa husika kuarifu wizara mara moja kuhusu mtu atakayepatikana akiwa na kiwango ha juu zaidi ya hicho, kwa kupiga simu kupitia nambari 719 ili kupata mwongozo zaidi.

Post a Comment

0 Comments