tangazo

Virusi vya Corona: Kuganda kwa damu, tatizo linalowakumba wagonjwa wengi walio katika hali mahututi lazua hofu

Wongonjwa wengi ambao wamekuwa na tatizo la damu kuganda katika mishipa wamekuwa wakitumia dawa za kujaribu kuyeyusha damu

Wangonjwa wengi ambao wamekuwa na tatizo la damu kuganda katika mishipa wamekuwa wakitumia dawa za kujaribu kuyeyusha damu hiyo na kufanya tatizo hilo lisilo la kawaida kuwa la kipekee.

Huku idadi ya wagonjwa waliopo na waliofariki ikiongezeka, madaktari wamegundua kwamba Covid-19, ugonjwa unaosababisha virusi vya corona ni ugonjwa usiofahamika kwa rahisi zaidi ya ilivyodhaniwa.

Ugonjwa huo unaweza kuathiri viungo kama vile ini, figo, utumbo, moyo na ubongo.

Tatizo kubwa lakini ni jinsi damu inavyoganda katika mishipa ya wagonjwa wanaopewa dawa za kufanya migando hiyo ya damu kuyeyuka.

Migando hiyo ya damu inaweza kufika katika viungo kama vile mapafu, moyo, ubongo na kusababisha mshtuko wa moyo unaoweza kusababisha kifo.

Siku chache zilizopita, madaktari katika hopsitali ya Mount Sinai mjini New York walichapisha utafiti unaosema kwamba mgando wa damu hususana katika mapafu unawaathiri vibaya wagonjwa wa Covid-19 walio mahututi.

Virusi vya corona: Je, Madagascar wamepata dawa ya mitishamba kutibu virusi vya corona?

Wataalamu hao pia walifichua kwamba migando hiyo ya damu inaweza kusababisha ugonjwa wa kiharusi miongoni mwa wagonjwa vijana walioambukizwa virusi vya corona.

Madaktari katika mataifa tofauti wameripoti tatizo sawa na hilo.

Uchanganuzi wa wagonjwa 183 wa Covid-19 uliofanywa na wanasayansi wa China umebaini kwamba asilimia 71 ya wale waliofariki walikuwa na mgando wa damu.

Nchini Uholanzi utafiti uliofanyiwa wagonjwa 184 waliokuwa wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi thuluthi moja ya wagonjwa hao walikuwa na mgando katika damu.

Coronavirus inaweza kuathiri sio tu mfumo wa kupumua lakini pia viungo vingine kama vile ini, figo, matumbo, moyo na ubongoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionCoronavirus inaweza kuathiri sio tu mfumo wa kupumua lakini pia viungo vingine kama vile ini, figo, matumbo, moyo na ubongo

Nchini Marekani madaktari wengi wamesema kwamba migando hiyo ndio sababu kuu ya vifo miongoni mwa wagonjwa wa Covid 19.

Ijapokuwa migando ya damu sio tatizo lisilo kuwa la kawaida kwa wagonjwa walio katika hali mahututi, maafisa hao wa afya wameshangazwa na idadi ya wagonjwa wa Covid 19 walio na tatizo hilo.

Je tatizo hilo husababishwa na nini?

Bado hakuna uamuzi wa pamoja kuhusu sababu za migando hiyo ya damu katika mishipa . Kufikia sasa kuna uvumi chungu nzima , alisema Coopersmith mtaalam wa chumba cha wagonjwa mahututi na profesa wa chuo kikuu cha tiba cha Emory University School mjini Atlanta, USA, akizungumza na BBC Brazil.)

Anasema kwamba kuna sababu nyingi ambazo lazima ziweko kwa damu kuganda na mwili hushindwa kuamua kati ya kuvuja damu na kuganda kwa damu hiyo.

Haijulikani iwapo migando hiyo husababishwa na virusi vya corona ama kinga katika hali yake ya kukabiliana na Covid-19.

Wagonjwa wengi huwa wamelazwa hivyobasi inaongeza hatari ya damu kuganda.


Post a Comment

0 Comments