Virusi vya corona: Umoja wa Afrika kuchunguza ufanisi wa dawa ya mitishamba ya Madagascar


Rais wa Madagascar Andry Rajoelina kushiriki kikao cha AU cha wakuu wanchi ambapo aliwafahamisha wenzake kuhusu dawa hiya ya Madagascar anayoamini inazuia na kutibu virusi vya corona.

Umoja wa Afrika (AU) unafanya mazungumzo na Jamuhuri ya Madagascar, ili kupata data za kiufundi kuhusu usalama na ufanisi wa dawa ya mitishamba iliyotangazwa hivi karibuni ambayo ilidai inazuwia na kutibu Covi-19.
AU imesema kuwa Kamishna wa tume ya Umoja wa Afrika inayohusika na masuala ya kijamii Amira ElFadil alifanya mazungumzo na balozi wa Madagascar nchini Ethiopia Eric Randrianantoandro tarehe 30 April na wameafikiana kuwa nchi wanachama wataupatia maelezo muhimu Muungano wa Afrika kuhusu dawa za mitishamba.
Baada ya kupata maelezo Umoja wa huo kupitia kituo chake cha udhibiti wa magonjwa - (Africa CDC), kitatathimini data zilizokusanywa kuhusu usalama na ufanisi katika tiba hizo asili dhidi ya virusi vya corona.
Dawa hiyo inayohusishwa na mmea wa Kichina unaoitwa Artemisia (pakanga) - ambao ni mojawapo ya miti ambayo huchanganywa pamoja na mimea mingine ya Madagascar kama tiba ya ugonjwa wa Malaria.

Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa cha Muungano wa Afrika (Afrika CDC) kitachunguza ufanisi na usalama wa mitishamba ya madagascar inayodaiwa kukinga na kutibu coronaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKituo cha Udhibiti wa Magonjwa cha Umoja wa Afrika (Afrika CDC) kitachunguza ufanisi na usalama wa mitishamba ya madagascar inayodaiwa kukinga na kutibu corona

Africa CDC ni taasisi ya Umoja wa Afrika inayosaidia nchi wanachama katika juhudi zao za kuimarisha mifumo ya afya na kuboresha uchunguzi, kukabiliana na dharura za magonjwa, kuzuwia na kudhibiti magonjwa.
Hata hivyo AU imesema kuwa tathimini yake ya madawa ya mitishamba itazingatia maadili ya kiufundi ya kidunia katika kukusanya ushahidi muhimu wa kisayansi kuhusu ufanisi wa mitishamba.
Hatua hii ya Umoja wa Afrika inakuja baada ya rais wa Madagascar Andry Rajoelina kushiriki kikao cha AU cha wakuu wan chi ambapo aliwafahamisha wenzake kuhusu dawa ya miti shamba ya Madagascar anayoamini inazuwia na kutibu virusi vya corona.
Hatua hiyo inawadia wakati ambapo marais karibu wanne wa Afrika wamesema wanaagiza kiasi kikubwa cha dawa ya mitishamba iliyosemekana kupatikana huko Madagascar kuwa ina uwezo wa kutibu virusi vya corona.
Marais wa Tanzania, Jamuhuri ya Congo, Guinea Bissau na Equatorial Guinea wote wamemaua kutuma ndege nchini Madagascar kuchukua dawa hiyo ya mitishamba.
Dawa za mitishamba ambazo mara nyingi hupatikana katika eneo huchangia pakubwa katika suala la afya kote barani Afrika.

Madagascar tayari imekwishasema itafanyia majaribio dawa yake

Hayo yanajri wakati Rais wa Madagascar akisema nchi yake itaanza majaribio ya kitabibu ya kinywaji cha mitishamba ambacho anakipigia upatu kuwa kinauwezo wa kuzuia na kutibu corona.
Rais Andry Rajoelina amesema majaribio hayo yataanza wiki ijayo.

Rais anawataka watafiti kuja na tiba ambayo 'waliipata kwamuda muafaka'Haki miliki ya pichaAFP
Image captionRais anawataka watafiti kuja na tiba ambayo 'waliipata kwamuda muafaka'

Pia amewataka wananchi wa taifa hilo kupanda kwa wingi mmea ambao unatomika kutengeneza kinywaji hicho. Kilichopewa jina la Covid-Organics.
Rais Rajoelina amesema kwa sasa anatafuta kibali cha WHO ili wathibitishe kinywaji hicho kuwa dawa.
Hata hivyo msimamo wa WHO kuhusu kinywaji hicho mpaka sasa haujabadilika na wanaonya watu dhidi ya dawa mbadala kutumika kama kinga ama tiba ya corona.
Mpaka kufikia sasa, watu zaidi ya milioni 3.5 duniani kote wamethibitishwa kupata maambukizi ya virusi vya corona, watu zaidi ya 250,000 (laki mbili na hamsini) wamefariki dunia huku watu zaidi ya milioni moja wakipona.
Tanzania kutuma ndege Madagascar
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli Jumapili ya Mei 3 alisema kuwa atatuma ndege Madagascar kwenda kufuata dawa ya hiyo mitishamba.
Magufuli amesema kuwa amewasiliana na Madagascar baada ya kupokea barua rasmi kutoka nchi hiyo iliyoeleza kuwa wamegundua dawa ya corona.
"Ninawasiliana na Madagascar na wameshaandika barua. Wanasema kuna dawa zimepatikana kule, tutatuma ndege kule na dawa zile zitaletwa pia ili Watanzania nao waweze kufaidika nayo… Sisi serikali tupo tunafanya kazi usiku na mchana."
Hatua hii ya Muungano wa Ulaya inakuja wakati Shirika la Afya Duniani (WHO) limesihi watu kutoweka imani zao kwa dawa za mitishamba zinazotengenezwa na wenyeji kwa misingi ya kudai kukabiliana na virusi vya corona.
Shirika la Afya Duniani limesema ni muhimu dawa zinazosemekana kuwa na uwezo wa kutibu kufanyiwa majaribio kwanza na kuonya kuwa huenda watu wakaona wamepata tiba na kujihisi kuwa salama ikiwa watakuwa na imani na dawa ambazo hazijafanyiwa majaribio.

Unaweza pia kutazama:




Virusi vya corona:Vidokezo tano ya jinsi ya kuimarisha afya yako ya kiakili

Post a Comment

0 Comments