tangazo

Virusi vya corona: Ushauri wa afya unaopotosha

Wengine wanadai kwamba mafuta ya haradali ni tiba ya corona

Wakati nchi duniani zikipambana na virusi vya corona, kumekuwepo na kusambaa kwa kiasi kikubwa kwa ushauri wa kiafya, ulio hauna maana lakini usio na madhara mpaka ushauri ambao unaweza kuwa wa hatari.

Tumekuwa tukitafuta baadhi ya mifano na kile ambacho sayansi inasema kuhusu hayo..

Kunywa pombe hakutazuia virusi

Tumekuwa tukitafuta baadhi ya mifano na kile ambacho sayansi inasema kuhusu hayo.

Kunywa pombe hakutazuia virusi

Hii imekuwa ikijitokeza mara kwa mara lakini inapotosha na ina madhara vilevile.

Mwanasiasa mmoja aliamuru kufunguliwa kwa maduka yanayouza vilevi, yaliyofungwa wakati wa amri ya kutotoka nje nchini India .

''Kama virusi vya corona vinaweza kuzuiwa kwa kunawa mikono kwa kutumia pombe, hivyo kunywa kilevi hakika kutaweza kuviondoa virusi hivyo kwenye koo,'' alisema Gharat Singh, mwanachama mwandamizi wa chama cha Congress, katika jimbo la Rajasthan.

Congress MP tweet

Lakini hakuna ushahidi wa kitabibu kuhusu hilo.

Na Shirika la afya duniani, WHO imeweka wazi kuwa kunywa kilevi si njia ya kuzuia virusi na njia hii inaweza kukuweka katika hatari ya kupata matatizo mengine ya kiafya.

WHO na vyombo vingine vya masuala ya afya huzungumzia pombe kama viambata vilivyomo kwenye vitakasa mikono

Kubana pumzi hakuwezi kukujulisha kama una virusi

Madai ya kuwa kubana pumzi huaminika katika nchi nyingi

Mtaalamu maarufu wa yoga nchini India, Baba Ramdev, amesema jaribu kuzizuia pumzi zako kwa dakika moja kama ni kijana na mwenye afya njema- sekunde 30 kwa watu wazima na wale wenye matatizo mengine ya kiafya.

Kama huwezi, anasema inaashiria kuwa una virusi.

Lakini hakuna ushahidi wa kisayansi ambao ni msingi wa madai haya.

Screen grab of image of Baba Ramdev

Mafuta ya haradali si tiba ya ufanisi

Vilevile mtaalamu huyo wa mazoezi ya yoga amesema kuweka matone ya mafuta ya haradali puani-mafuta hutoa virusi nje ya mfumo wa upumuaji na kuelekea tumboni ambapo virusi vitakufa kwa asidi.

Dawa ya kuua vijidudu na miale ya urujuanimno (UV light)

Tangu Rais wa Marekani Donald Trump alipotoa wazo mwezi uliopita kuwachoma sindano wagonjwa kwa kutumia kemikali na kuwa huenda ikasaidia kutibu corona, wazo hililimekuwa likizungumzwa mitandaoni katika nchi nyingi.

Image of bleach bottle

Kutumia dawa ya kuua vijidudu kunaweza kuua virusi kwenye maeneo mbalimbali , lakini kuitumia kwa kumchoma mtu kunaweza kumfanya awe katika hatari ya kupoteza maisha.

Pia hakuna ushahidi wowote kuhusu ufanisi wake dhidi ya virusi.

Trump pia amezungumzia kuhusu kuwachoma mionzi wagonjwa.

Na kuna ushahidi kuwa virusi haviishi kwa muda mrefu kwenye vitu vinapopatwa na mwanga wa jua wa moja kwa moja.

Lakini ni hatua hii huwa na madhara kwa tishu za binadamu.

Hakuna ushahidi wa kisayansi kuwa mwanga wa urujuanimno una ufanisi katika kutibu mtu mwenye virusi vya corona.

Post a Comment

0 Comments