Virusi vya corona: Vijana Kenya wavumbua mfumo wa CovIdent unaotarajiwa kutambua wote wenye virusi

Mhandisi Bundi Kotonya, aliyeongoza kikosi cha uvumbuzi wa CovIdent, anasema Mfumo huu unaweza kutambua maeneo yotealikoenda mtu na watu aliokutana nao.

Tangu kuibuka kwa virusi vya corona, juhudi mbali mbali zimekua zikifanyika ili kuzuwia kusambaa kwa virusi ambavyo vinaambukizwa kwa kasi duniani na kusababisha vifo.

Katika juhudi za Chuo kikuu cha Teknolojia cha Serikali cha Meru nchini Kenya kimevumbua mfumo wa kidigitali unaofahamika kama CovIdent utakaotoa alama za data binafsi kwa lengo la kurahisisha upimaji wa virusi vya corona kwa watu wengi.

Uvumbuzi huu umefanywa na Wahandisi vijana Chuoni hapo wanaotambulika kama NaiTech chini ya usimamizi wa mhandisi Bundi Kotonya.

Mfumo utasaidia kuwapa watu nafasi ya kupata, kunakili na kutumia matokea ya upimaji wao kwa njia rahisi.

Mfumo huu utasaidia kuwatambua na kuwachuja wenye maambukizi ya virusi vya corona na hivyo kupunguza kuenea kwa Covid-19 ambapo baada ya mtu kufanyiwa vipimo vya corona mfumo utaweka alama maalumu ya siri (code) na kutuma maelezo yake katika kituo cha taifa cha udhibiti wa corona au ugonjwa mwingine ambapo maelezo hayo yatahifadhiwa.

''Alama yako ya kidigitali unaweza kuitumia popote kuonyesha hali yako ya kiafya kuhusiana na corona'', anasema Profesa Romanus Odhiambo, aliyeongoza mpango wa uvumbuzi wa CovIdent na kuongeza kuwa unapotaka kwa mfano kuitumia kazini au mahala pengine unapohitajika kutambulisha afya yako kuhusu corona mfumo wa CovIdent utakutambulisha kwa njia ya alama ya siri.

Vijana walioshiriki katika Chuo Kikuu cha teknolojia cha Meru waliovumbua mfumo wa CovIdent wanasema kuwa unaweza kusaidia kutumika kutunga sera za afya dunianiHaki miliki ya pichaCHUO KIKUU CHA TEKNOLOJIA CHA MERU
Image captionVijana walioshiriki katika Chuo Kikuu cha teknolojia cha Meru waliovumbua mfumo wa CovIdent wanasema kuwa unaweza kusaidia kutumika kutunga sera za afya duniani

CovIdent unaweza kutambua mtandao wa watu ambao mtu amekutana nao na hivyo kutambua wagonjwa na watu wenye uwezekano wa kuambukizwa virusi vya corona baada tu kukutana na mtu mwenye maambukizi.

''Mfumo huu unaweza kutambua maeneo yote ulikoenda na watu uliokutana nao, na hivyo unapopata taarifa zote hizi inakua rahisi kudhibiti maambukizi zaidi'', anasema Mhandisi Bundi Kotonya, kiongozi wa vijana wavumbuzi CovIdent, katika Chuo Kikuu cha Meru.



Kulingana na Chuo Kikuu cha Meru mfumo huu wa kidigitali umebuniwa kwa ajili ya kuimarisha vita dhidi ya Covid-19, kwa kupunguza kuenea kwa virusi hivyo nchini Kenya na Afrika kwa ujumla.

Kutokana na kwamba CovIdent inaweza kuweka kutambulisha data za mtu binafsi za matibabu, Chuo Kikuu cha Meru kinatumai kuwa unaweza kusaidia kutumika kutunga sera za afya duniani hususan kuhusiana na magonjwa maambukizi.

Kadi hizi za CivIdent zinatarajiwa kutunza data za mtu kwa ajili ya utambuzi wa hali yake ya kiafya kuhusu virusi vya coronaHaki miliki ya pichaCHUO KIKUU CHA TEKNOLOJIA CHA MERU KENYA
Image captionKadi hizi za CivIdent zinatarajiwa kutunza data za mtu kwa ajili ya utambuzi wa hali yake ya kiafya kuhusu virusi vya corona

Je matumizi ya CovIdent sio hatari kwa data binafsi.

Kulingana na Taasisi ya Chuo Kikuu cha Meru, uvumbuzi huu unaambatana na sera ya serikai ya Kenya ya ulinzi wa data za kibinafsi: ''Chuo Kikuu cha Meru ni cha serikali data za mtu binafsi haziwezi kufichuliwa na ndio maana uvumbuzi huu umefanyika hapa na si katika taasisi binafsi ili kulinda data binafsi'', anasema Daniel Bundi Kotonya, kiongozi wa uvumbuzi huu.

Uvumbuzi huu unalenga kuiwezesha jamii kurudi katika hali ya kawaida kwa utaratibu, kwa kudhibitiwa, kuthibitishwa kwa njia ya kupimimwa na iliyo ya faragha, ameongeza Daniel Bundi.

Kikosi Cha vijana wa NaiTech pamoja na Kaimu Mkuu was Chuo hicho Technologia Cha MeruHaki miliki ya pichaCHUO KIKUU CHA TEKNOLOJIA CHA MERU
Image captionKikosi Cha vijana wa NaiTech pamoja na Kaimu Mkuu was Chuo hicho Technologia Cha Meru, wanamatumaini kuwa CovIdent itawawezesha watu kuendelea na shughuli zao bila hofu ya maambukizi ya virusi vya corona.

Je mfumo wa CovIdent unafanyaje kazi?

  • Matokeo ya Kupimwa kila mtu yatakuwa na alama maalum ya kidijitali ambayo itakuwa kwenye Jukwaa Maalum litakalodhibitiwa na serikali.
  • Kila atakayekuwa amepimwa atapata alama maalum (Digital Code) ambayo itakuwa kitambulisho cha kuruhusu kujumuika na wengine kama yeye katika sehemu za kazi.
  • Alama hii maalum (digital code) itasomeka kupitia kwa simu ya kawaida kwa kutuma ujumbe mfupi (USSD) na matokeo yatapatikana mara moja.
  • Kwa kutumia simu nyingine za rununu alama hii maalum itasomeka kwa kupitia camera inayojulikana kama QR.
  • Mfumo huu wa CovIdent utatumiwa kufuatilia wagonjwa wapya kwa kutoa taarifa za technolgojia kwa kutuma ujumbe mfupi kwa Kitengo maalum.Taarifa zaidi za corona:
Virusi vya corona:Vidokezo tano ya jinsi ya kuimarisha afya yako ya kiakili

Post a Comment

0 Comments