tangazo

Virusi vya corona: Wachezadensi wanaosindikiza wafu waliopenda mtandaoni

Mwaka 2017 kikundi hiki cha wachezajidensi cha Ghana wanaosindikiza wafu walipata umaarufu baada ya BBC kufanya taarifa juu ya densi yao maarufu yenye mvuto ya kubeba jeneza , iliyotazamwa na mamilioni ya watu.

Miaka mitatu baadae kikundi hiki kimepata umaarufu wa kimtandao kwa mara nyingine tena, huku watumiaji wa mitandao ya kijamii wakitumia densi ya kikundi hicho kama mzaha kuelezea kuhusu kifo wakati huu wa Covid-19.

Mwandishi wa BBC Africa Sulley Lansah alikutana na kiongozi wa kikundi kupata maoni yake juu ya umaarufu mpya walioupata na kujionea jinsi anavyoendelea wakati huu wa janga la corona.

Tazama Video Hapa Chini

Post a Comment

0 Comments