Virusi vya corona:Daktari mkuu aonya kuhusu uwezekano wa kusambaa zaidi kwa Covid-19 Marekani

Daktari wa ngazi ya juu wa Magonjwa ya maambukizi nchini Marekani amewaonya maseneta kuwa virusi vitasambaa iwapo nchi itafungua shughuli zake mapema sana.
Dkt Anthony Fauci amesema kuwa miongozo ya shirikisho ya kufungua shughuli za kibiashara tena haitafuatwa , "maambukizi madogo madogo" yatakua mlipuko.
Amesema pia kwamba idadi halisi ya vifo nchini Marekani huenda ikawa kubwa kuliko idadi rasmi inayotolewa ya vifo 80,000.
Ujumbe wake uko kinyume na taarifa iliyotolewa na rais Trump ambaye yuko makini kutaka shughuli za kiuchumi zifunguliwe tena.


ADVERTISEMENT


Dkt. Fauci alikua akizungumza kwa njia ya video na kamati ya seneti inayoongozwa na Republican nchini Marekani.
Alikua akielezea kuhusu mpango wa kufunguliwa upya kwa shughuli Marekani baada ya majimbo zaidi ya kumi na mbili kuweka amri ya kukaa nyumbani ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona ,ambao unajumuisha awamu ya siku 14 ambazo majimbo yanaombwa kuzifuata wakati wanaporuhusu kufunguliwa kwa shule na biashara.
Majimbo kadhaa ya Marekani ambayo tayari yamekwishaanza tena shughuli zao za kiuchumi yana viwango vya juu vya ongezeko la maambukizi, badala ya kushuka.
Omeonya kuhusu kusababisha mlipuko ambao maafisa hawataweza kuudhibiti, akiongeza kuwa mlipuko wa aina hiyo utarudisha nyuma kufufuka kwa uchumi na unaweza kusababisha "kuugua na vifo".
Ingawa ikulu ya White House imeweka miongozo ya kufungua shughuli za kiuchumi , ni jukumu la magavana kuamua juu ya namna ya kulegeza sharia za kukaa nyumbani zilizowekwa.
"Bila shaka, hata katika hali nzuri sana, ukipunguza hatua za kudhibiti maambukizi utaona visa vinajitokeza ," Dokta Fauchi aliwaonya maafisa wa Mrekani

''Matumaini ya tahadhari'

Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kurejea tena wa virusi wakati wa majira ya vuli, Dokta Fauci alisema "inawezekana au isiwezekane".
"Ninatumai kwamba kama tuna tisho la wimbi la pili tutaweza kukabiliana nalo kwa ufanisi zaidi kama utakuwa mlipuko."
Dokta Fauci pia alisema kuwa kuna chanjo nyingi ambazo zinatengenezwa lakini "hakuna uhakika" yoyote itakuwa na ufanini, ingawa kwa misingi ya uelewa wake wa virusi vingine, ana "matumaini lakini kwa tahadhari".
"Tuna nyingi zinazofanyiwa uchunguzi na natumai zitaweza kufikia viwango hitajika,"alisema. "Kwa maneno mengine ni suti nyingi za goli."

Mashahidi walitoa ushahidi kwa njia ya video

Mashahidi walionekana kwa njia video kwakati wa kikao cha zaidi ya saa tatu, sawa na walivyofanya maseneta wa Kamati ya Masuala ya Afya, Elimu na Malipo ya uzeeni.
Wajumbe watatu wa kikosi kazi cha kupambana na virusi vya corona cha ikulu ya White House walitoa ushahidi wao wakiwa karantini baada ya kuwa na uwezekano wa kuugua mkiwemo Dkt. Fauchi.
Mkurugenzi wa Vituo vya Kuudhibiti na Kuzuwia ugonjwa Centers for Disease Dokta Robert Redfield na kamishna wa taasisi ya Mareakni ya Utoaji wa Stephen Hahn pia wamejitenga binafsi kutokana na uwezekano wa kupata maambukizi ya virusi.
Dkt. Fauci hakupatikana na virusi alipopimwa lakini ataendelea kufanyia kazi nyumbani kwa sasa, na atakuwa akipimwa mara kwa mara.


Banner

Kikao kiliongozwa na seneta wa Republican kutoka jimbo la Tennessee Lamar Alexander akiwa nyumbani kwake eneo la Smoky Mountains. Mbwa wake aina ya Rufus alikua akionekana mara kadhaa akizunguka nyuma yake wakati wa kikao cha njia ya video.
"Kukaa nyumbani daima sio suluhu la janga hili ," alismea Bwana Alexander, na kuongeza kuwa "Hakuna pesa za kutosha zilizopo za kuwasaidia wale wote wanaoumizwa na kufungwa kwa shughuli za kiuchumi."
Seneta wa Washington Patty Murray, mwenye cheo cha juu katika kamati ya Democratic, alikasirika kwamba Bwana Trump anataka zaidi "kupambana zaidi na ukweli kuliko kupambana na virusi ".
Serikali haiwezi kuwaomba watu kuanza upya maisha yao ya kawaida "kama hakuna maelezo ya wazi ya muongozo juu ya jinsi ya kufanya hilo kwa usalama ", aliongeza.
Wakati huo huo Makamu rais Mike Pence pia yuko mbali na rais Trump baada ya afisa wake wa habari Katie Miller kupatikana na virusi vya corona baada ya kupimwa wiki iliyopita.
"Makamu wa rais amefanya chaguo lake la kukaa mbali kwa siku chache," alisema afisa wa habari wa White House Kayleigh McEnany.

UCHAMBUZI

Ushahdi wa Anthony Fauci mbele ya kamati ulianza kama mazungumzo ya kawaida ya busara, huku maseneta wakimchukulia kama afisa wa huduma za afya wa muda mrefu ambaye ushauri wake unaonekana una mamlaka na wenye utaalamu.
Halafu Seneta Rand Paul alizungumza
Inapokuja katika suala la virusi vya corona, mwanasiasa huyo wa Republican kutoka Kentucky alisema, wataalamu wa afya ya umma walifanya "ubashiri wa kimakosa baada utabiri wa makosa baada ya ubashiri wa makosa ".


ADVERTISEMENT


"Ingawa ninakuheshimu Dokta Fauci," aliendelea, "Haukufanya maamuzi mazuri yote, Sidhani ulikua mtu wa kuweza kufanya maamuzi ."
Bwana Paul alikua akiunga mkono hisia zinazoendelea kushamiri miongoni mwa mahafidhina kwamba Dokta Fauci hhaweki mbele maslahi ya taifa sana sawa na raisTrump.
Umati wa wanaharakati wanaopinga amri ya kukaa nyumbani katika majimbo kadhaa ulishangilia "fukuza Fauci", na mkurugenzi aliomba ulinzi maalumu baada ya kupokea vitisho vya kuuawa. Wao, sawa na Bwana Paul wamepuuzilia mbali kuenea kwa virusi zaidi ya maeneo ya sasa ya mwambao ye vitovu vya mlipuko, ingawa data zilizopo zinaonyesha visa vimepanda juu katika baadhi ya maeneo ya ndani ya Marekani.
Ni ushahidi wa kuongezeka kwa mgawanyiko wa kisiasa ndani yataifa juu ya jinsi ya kukabiliana na virusi na ni lini, wanapaswa kuanza kulegeza amri zilizopo kwa sasa za juhudi za kudhibiti maambukizi ya virusi.
Dokta Fauci, kwa upande wake, alijibu kwa upole.
"Sijawahi binafsi kuwa kauli ya mwisho na sauti pekee ya jambo hili ," alimuambia Bwana Paul. "Mimi ni mwanasayansi, mwanafizikia na afisa wa afya wa umma."
Aliongeza kwamba bado kuna mrengi ambayo hayajafahamika kuhusu virusi.
Dokta Paul ambaye binafsi alipatikana na maambukizi ya virusi vya cokrona mwezi uliopita alipata ukosoaji mkubwa kwa kuendelea kufanya kazi katika seneti na kuwaweka wenzake hatarini kwa kufanya kazi baada ya kutambua kuwa alikua na virusi.

Post a Comment

0 Comments